Header Ads

AFCON 2017: Kahraba Aipeleka Misri Nusu Fainali

Mabingwa wa kihistoria barani Afrika, timu ya taifa ya Misri wamekamilisha idadi ya timu nne zitakazocheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya AFCON 2017 inayoendelea nchini Gabon, kwa kuifunga Morocco bao moja kwa sifuri.
Bao lililofungwa na kiungo mshambuliaji wa klabu ya Zamalek anaecheza kwa mkopo Al-Ittihad ya Saudi Arabia Mahmoud Abdel-Moneim * Kahraba (Umeme)* lilitosha kuipeleka Misri kwenye hatua ya nusu fainali.
Pamoja na kikosi cha Morocco kuonyesha soka safi katika kipindi cha pili, bado hali ilikua ngumu kwao, kufanikisha azma ya kusawazisha na mambo yaliendelea kuwa magumu hadi mtanange huo ulipomalizika.
Ushindi wa bao moja kwa sifuri umeisogeza Misri pembezoni mwa Burkina Faso ambao watapambana nao kwenye hatua ya nusu fainali siku ya jumatano.
Wakati huo huo Ghana walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Congo DR katika mchezo wa robo fainali uliounguruma saa moja jioni kwa saa za Afrika mashariki.

Ghana watapambana na Cameroon katika hatua ya nusu fainali siku ya Al-khamis. 

No comments

Powered by Blogger.