Header Ads

ZEE L NYETI: Hakuna cha Ukata, dili tata zimeweka ukuta!

Ebana mambo VP?
…kitambo enh?
naskia kitaa huko mlishaanza kupitisha daftari la michango, mnawaambia wanangu nimededi sasa mnaumbuka. Nimerudi mtu mzimakwa kasi ile ile ila sasa nimeamua kupitisha ishu kwenye waya. Kule kwenye pepaz kama wana wamezingua flani hv, nikaamua kuja kuzimwaga huku najua wale wanangu wa damu wataunga tela tu.

Big Up kwa wanangu waliosisitiza Zee lirudi Onlaini, …akin Danny Mzena, Mohamed Chande a.k.a Dijei Kyuu,wanangu mwenyewe Kareem Tembele na wana kibao. Saskia staili wana wameikubali kwa hiyo wameibuka weeeengi. Ilahuu moto si mnaunyaka wanangu? 
…unafaa kuigwa?
Watonyeni basi wanaadhirika mwaka huu….

Half naskia kitaanikimenuka, kila mchizi anamlalamikia mtu mzima Ngosha,kwamba kabana ishu zimekuwa ngumu na nini.Wengine ndio wanazingua kile chama kilichompitisha kwamba ishu za kuisoma namba ndio zimekuwa civiele, ..naskia yaani nomakitaani, bongo mwanangu?
…najua ushaitikia ndio….
Mnakawia kwani nyie kwenye kujiliza?

Zee kama ze simonie kama ishu zimekuwa ngumu mwanangu mwenyewe, ila sasa zile ishu tata dile ndio zimekata na tata ndio unaanzia hapo. Halafu mwanenu huwezi kuamini naona poa tu, acha tunyooshwe, …tulizidi.

Acha ijulikane sasa mwenye buku nani, na mwenge mia nani, potelea mali ila heshima iwepo.

Ujue mwanangu ilifikia kipindi watoto wadogo wenye dili tata tauni walikuwawanazingua kitaa mpaka tukatamani kuhama nchi. Watoto wanatunzingulia mpaka waifu zetu na mikwanja yao feki wakati watu wazima tulikuwa tunamenyeka kuweka ishu sawa.

Mimi kuna mwanangu aliporwa waif wake hivi hivi.

Jamaa kasomesha mchumba nini, …inafika wakati chumba kamaliza makoleji ndio anarudi homu, Mzee wa dili tata akamuona akazama kwa washua wa yule demo unaambiwa. Acha atembeze mikwanja, washua wakadata,wakapigwa suu kwamba mchizi akiibuka mpeni za mbavu. 

Basi unaambiwa ile schizzi anaibuka kuweka sawa mambo ya Posa sijui mahari watu wakamkazia. Ile analeta kompleini sijui za kwamba kamsomesha demu nini watu wakamwambia piga hesabu zako, wakamuwekea mkwanja wake mezani na bonasi wakampa.

Unanisoma mwanangu?

Sio hadithi, tru stori….

Unaambiwa huku na huku, mchizi akaona sio ishu, akauvuta ule mkwanja kwanza, akasepambele kwa mbele half huyo mwanangu dizaini mangi, Basi na mji akauona mcuhngu, akazama zake Kiboroloni akafungua goli, maisha yakaendelea.

Eliza nini sasa…

Hivi tunavyopiga store mwanangu mwenyewe, yule Mzee wa Dili tata wakati ananyooka, mwanangu ndio anashaini sasa, halaf ndoa yenyewe alizuga, hakumuoa yule demu. Wakati wake katika kula yale magudtamu, Ngosha si akaingia madarakani?

Ijshut zikaanza kukata moja baada ya nyingine kumbaambeki!

Halaf kule mwanangu Mangi kijliwe ndio kimechanganya, utamueleza nini?

Mzee wa dili tata kupunguza kosti za maisha imebidi ampige chini demu kwanza akomae na familia, huyu demu si alitaka shotikati? Unadhani atasemaje kipindi hiki, si ataona kuna kata?

Na yule mchizi, atampenda Ngosha kweli? Ila watu wenye ishu zilizonyooka kamakawa viti virefu tunakaa na gambe tunapiga na watoto wakali tunach’kua. UongoMwanangu mwenyewe?

Kata ni kwa wenye dili tata lakini wenye ishu zilizonyooka tunapeta!

Basimwanangu hii kila Chuzdei, ntakuwa naidondosha hapa Zee la Nyeti limerudi waambie washkaji kitaani wanicheki na usiache kuacha maoni yako ukimaliza kusoma hapo chini au sio?


Nakuaminia

No comments

Powered by Blogger.