Header Ads

UNA HABARI? Kuna sehemu umeme utakosekana kesho

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Geita, Mara, Simiyu na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya  Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga

Kia jiji la Dar es Salaam (Tazara, Mlimani City, Mandela Road, Ubungo na Kimara, Sinza, Mabibo) kuwa yatakosa Umeme siku ya Jumapili DESEMBA 04, 2016 kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni.

SABABU: Kuruhusu Mkandarasi anayejenga Njia Kuu ya Kusafirisha Umeme ya Msongo Mkubwa ya Kilovolti 400 maarufu kama (Backbone Transmission Line 400 kV) kutoka Iringa hadi Shinyanga.

SABABU: Kuzimwa kwa njia ya Umeme ya Msongo wa Kilovolti 33 Kituo cha Ubungo Dar es Salaam ilikumruhusu Mkandarasi kufanya matengenezo.

Matengenezo hayo yanalenga kuboresha na kuimarisha hali ya upatikanaji wa Umeme Nchini.
  
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na; Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu

PICHNI JUU: Mhandisi wa umeme wa Shirika la Umeme nchuini Tanzania TANESCO, akiwa kazini jijini Dar es Salaam


No comments

Powered by Blogger.