Header Ads

Timu ya Chapecoense yatunukiwa kombe la Copa Sudamericana


Klabu kadha Brazil zimejitolea kuipa Chapecoense wachezaji
Klabu ya Chapecoense kutoka Brazil, ambayo iliwapoteza wachezaji 19 pamoja na wahudumu kwenye ajali ya ndege walipokuwa wakielekea kucheza fainali ya Copa Sudamericana, imetunukiwa kombe hilo.
Uamuzi huo umechukuliwa na shirikisho la soka la Amerika Kusini, Conmebol kufuatia ombi la wapinzani wa klabu hiyo.
Watu 71, wakiwemo wachezaji 19 na wahudumu wa klabu hiyo, walifariki Jumatatu wakielekea Colombia kwa mechi ya mkondo wa kwanza ya fainali ya kombe hilo.
Wapinzani wa klabu hiyo kutoka Atletico Nacional, ambao waliomba Chapecoense wapewe kombe hilo, wametunukiwa tuzo ya Uchezaji Haki ili kutambua "moyo wao wa amani, kuelewa na kucheza haki".
Chapecoense pia watapewa jumla ya $2m (£1.57m) ambazo hukabidhiwa mshindi.
Atletico Nacional nao watapewa $1m (£787,000).
Wachezaji watatu wa Chapecoense ni miongoni mwa watu sita walionusurika katika ajali hiyo.
Uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo unaendelea lakini sauti iliyonakiliwa na mitambo ya ndege hiyo inaashiria huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta kabla ya kuanguka karibu na mji wa Medellin.
Wachezaji wengi wa Chapecoense walifariki, pamoja na wanahabari 20 walioandamana nao

No comments

Powered by Blogger.