Header Ads

SOMA: Kuhusu Nikki Mbishi na jinsi anavyoweza kuvaa uhusika wa ngoma zake

Na John Simwanza
Nikki mbishi ndio jina analotumia katika kazi yake ya muziki ila sio mbaya hata Ukimwita Zohan,Baba malcom au Unju bin unuk Nikki atakuitikia bila shaka Nikki mbishi ni mwanafamilia harali kabisa wa Tamaduni muziki inayojihusisha na muziki wa Hip hop au Rap.

Nikki mbishi alijulikana zaidi kwa mashabiki wake na  kupendwa alipo achia ngoma yake iliyokwenda kwa jina la Playboy wakati huo akisimamiwa na prodyuza Duke katika lebal ya m-lab lebal iliyokua na wasanii kama vile One the incredibel,Stereo pamoja na mkali wa RnB nchini Ben pol.

Uwezo alionao wa kuuvaa uhusika wa ngoma zake umekua ukiwashangaza watu wengi na kupelekea kutokumuelewa atakuja vipi kwa ngoma zake za mbele hicho   pengi ndio ni miongoni mwa vitu anavyojivunia Zohan katika kuimudu vilivyo nafasi yake kwenye muziki huu ambao kila kukicha unakuwa na wageni wapya wanaotaka kuchukua nafasi za  wakongwe

Waandishi wa zamani wanatofauti kubwa sana na waandishi wa sasa kwa sababu wasanii wa wa zamani walikuwa wanaandika Mada  amabayo ndio ataizungumzia msanii katika kila verse lakini waandishi wa sasa wamejikita katika kutengeneza Hit na sio myimbo zinazoishi  na ndioana wanashindwa kuuvaa uhusika kutokana na nyimbo kutokua na mada moja.

Nyimbo nyingi za Nikki mbishi huwa hazitoki nje na mada husika hapa namaana ya kwamba jina la wimbo ndio kitu utakachokisikiliza na sio tu katika ngoma moja au mbili ambazo amefanya ivo ni takribani nyimbo zote hasa zile zinazokuwa ni rasmi kwenda Radio.

Niki mbishi amesha fanya ngoma nyingi ambazo umeuvaakiukamilifu uhusika hasa tukianza na 
           

NAY WA MITEGO
Jina la wimbo huu ndio jina la Rapa Emmanueli Elibariki katika kazi yake ya muziki alimaarufu kwa jina la nay wamitego ngoma hii ya Nikki mbishi ilichukuliwa tofauti sana na wengi wao wakaamini wazi kuw mbishi kamuimba nay tunaemjua lakini ukisikiliza kwa umakini utagundua nikki alikua anamuongelea binti flani ivi anae ishi manzese na kuuvaa uhusika wa kijana anaehitaji kuwa nae japokuwa nae nay wa mitego ambae ni neema anakuwa anamtega nikki. 
        

BABU TALENT
Ndio ngoma ya kwanza kutambulishwa kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii kabla haija rekodiwa studio kwa njia ya mashairi yake kuwa wazi na baada ya kutoka tu kwa babu talent Nikki aliuvaa uhusika kuanzia kwenye Audio mpaka video na kuionesha maeneo halisi kabisa anayotokea huyo babu talent ambae ni nikki mbishi.

SAUTI YA JOGOO

Ndio  ngoma iliyobeba Jina la Album yake ya kwanza utunzi wa hii ngoma angekua ndio msanii wa kawaida asinge cheza na maneno yanayoweza kumvisha uhusika kwani nikki ametengeneza nyimbo ya kutoa hamasa kwa kila mmoja katika kujituma na kufikiamalengo kwa njia ya kujivisha ujogoo ili kuwaamsha mapema kama ilivyo katika uhalisia wa maisha ya Jogoo.

Niwa sanii wachache sana ambao wanaweza kucheza na uhusika wa nyimbo zao bila kuhama nje ya mada wanayoizungumzia.

No comments

Powered by Blogger.