Header Ads

MZIKI WA DULLY UNASUKUMWA SANA NA WAKALI WA SASANA JO
HN SIMWANZA

Miongoni mwa nguli wa muziki huu wa kizazi kipya  walio utoa  huko mafichoni na kuuleta kwa wadau na mashabiki Dully Sykes a.k.a Brother man nae ni mmoja wapo.

Tokeo la picha la picha za dully sykes

Dully ni msanii wa mwanzo kabisa  alie toka kwenye ku rap na kuingia katika muziki wa kuimba(BongoFlava)  ambako mpaka sasa ndio amejikita na anaendelea kupamudu vilivyo.Dully ndio msanii aliekua ana sumbua sana katika club mbali mbali sio tu kwa kufanya show nyingi bali hata nyimbo zake zilikua zikitawala playlist za ma dj wengi wa club za usiku.

Tuna list kubwa sana ya wasanii wazamani waliokua wana hit na hawapo tena katika ramani na hata kama wakijitahidi kurudi basi pumzi yao inakua fupi kuliko safari wanayo takiwa kuikamilisha lakini kwa dully imekua ni tofauti kabisa  kwani mchezo anaucheza kama unavyotakiwa kuchezwa.

Kudumu kwake katika game kumekua na faida sana kwa wasanii wachanga kwani ana mchango mkubwa sana na baadhi yao wamekua hawasiti kumpa heshima yake na kutochoka kumzungumzia kwa mazuri alio wafanyia hasa Diamond,Mr Blue,Alikiba , Ommy Dimpoz na wengine wengi

Maneno bila vitendo ni sawa na kazi bure Wakali hawa wa sasa hawajawahi kumuangusha  kaka yao (Dully) katika swala zima la matendo Nae huwa hana choyo kuwapa nafasi katika kazi zake na ndio mana huwa wanatengeneza kitu kisicho tarajiwa sana na mashabiki wake ambao hawajutii kuwa nae katika safari hii walioanza nae miaka hiyo ya nyuma.

Tokeo la picha la picha za dully sykes

Ushirikiano  wa dully na wasanii wanaotamba kwa sasa hasa katika kazi umekua ukimpa mafanikio makubwa sana mkongwe huyu hasa katika show na hivyo kutudhihilishia kuwa mziki wake unasukumwa sana na wasanii wa leo. Siyazungumzi haya hivi hivi kwani nataka nikuthibitishie hili kwa kuzi angalia Ngoma Tatu alizoshirikiana na wasanii wanaotamba kwa sasa na zikasumbua kila kona ya nchi hii.


                DHAHABU
Ninaweza kusema dhahabu ndio ngoma iliyo kujakuwatofauti Blue na josiln style zao za kuchana kwani ukisikiliza kwa makini verse zao utagundua kila mmoja ana uwezo wake binafsi licha kuwa kama wanashabihiana kwa baadhi ya vitu katika muziki wanaofanya. Dhahabu ilidumu kwa kipindi kirefu sana katika chati mbali mbali na mara nyingi sana imechaguliwa na watu tofauti tofauti kama dedication kwa wapenzi wao.

                UTAMU
Ilipikw katika studio za 4.12 zinazomilikiwa na legend brother men Dully sykss nakuwakutanisha mafundi wa mziki huu kwa sasa  na wanaoongoza kwa kuwa na show nyingi sana za nje ya nchi hapa nawazungumzia members wawili wa  kigoma all star Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz  walitia baraka zao na kufanya kutoa gumzo jipya tena lililo mpeleka kileleni kwa mara nyingine tena Dully sykss katika ramani ya mziki Utamu ilikua kali sana kuanzia audio mpaka video yake.
Tokeo la picha la picha za dully sykes
                 INDE
Ndio ngoma inayofanya vizuri  kwa sasa kila kona aliyomshirikisha Harmonize msanii alieingia katika game nakujinyakulia tuzo mbili kubwa za Afrika Inde imekuja kwa kasi na kadri siku zinavozidi kwenda ndio sumu ya inde inazidi kuwadhoofisha wasanii wakali wa hivi sasa na kuwaacha midomo wazi wakongwe wenzake anaoishia kuwatimulia vumbi kila kukicha inde ndio ngoma inayosumbua chati takribani zote za hapa nyumbani.


Uhusiano mzuri wa dully na wasanii wa sasa ndio imekua ni kinga yake inayomlinda kila siku katika muziki wake na kwamwenendo huu tusitegemee kama tutakuja kumpoteza Nguli huyu katika ramani ya mziki hata game ibadilike vip najua atacheza nayo tu kwani siri ya huu  mchezo haipo tu kwa fid na juma nature siri hii hata Dully anayo. 

No comments

Powered by Blogger.