Header Ads

Mwandishi Soyinka aondoka marekani kabla ya Trump kuapishwa

Wole Soyinka
Mshindi wa  tuzo ya Nobel raia wa Nigeria Wole Soyinka, ametimiza ahadi ya kuirarua green card yake kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Mwezi uliopta mshindi huyo wa tuzo la fasihi alisema kuwa angeirarua green card yake, ambayo humpa mtu kibali cha kuishi nchini Marekanai ikiwa Donald Trump angechaguliwa kuwa rais wa Marekani.
Aliliambia shirika la AFP mjini Johannesburg kuwa kwa sababu Trump ameshinda, basi ametekeleza alichokisema
"Tayari nishafanya, nimetoka Marekani , nimefanya kile nilisema ningekifanya, nilitupa green card yangu , nimerudi penye ninastahili kuwa," alisema Soyinka.
Hata hivyo Soyinka hawashauri watu wengine kufuata mkondo huo.

No comments

Powered by Blogger.