Header Ads

MSHAMBULIAJI WA MBAO FC U-20 ISMAIL MRISHO AFARIKI DUNIA


Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao Fc U-20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki Dunia jana jioni baada ya kuanguka Uwanjani Kaitaba wakati wa Mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana. 
Ismail Mrisho Khalfan amefariki akiwa na miaka 19.
Ismail Mrisho Khalfan akipata huduma ya kwanza kutoka kwa madaktari wa Timu yake jana kwenye Uwanja wa Kaitaba. 
Akipata Huduma ya haraka baada ya kuanguka Uwanjani. 
Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao Fc U20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki Dunia jioni hii baada ya kuanguka Uwanjani Kaitaba wakati wa Mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana. 
Ismail Khalfan amefariki akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mjini Bukoba. 
Ismail Mrisho Halfan alifariki akiwa njiani kuelekea Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kagera iliyoko katika Manispaa ya Bukoba.
Mrisho Halfan ndie aliyeifungia bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.
ISMAIL MRISHO HALFAN wa tatu kutoka (kushoto) muda mfupi kabla ya Mtanange wao kuanza leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.
Ismail Khalfan kabla ya kufikiwa na umauti aliweza kuifungia timu yake bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0. 
Kabla ya kuanguka Ismail aligongana na beki wa Mwadui Fc na baadae akiwa peke yake alianguka chini lakini akainuka halafu akaanguka tena na kutokana na ukosefu wa huduma ya kwanza na gari la wagonjwa Katika Uwanja wa Kaitaba kulipelekea marehemu kupandishwa kwenye gari la zima moto na kupelekwa hospital ambapo mauti yalimkuta. 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. 

Mchezaji Ismail Mrisho Halfan wa timu ya Mbao U-20 akitolewa uwanjani na watu wa msalaba Mwekundu baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mchezo wao uliokuwa ukichezwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba

Mchezajiwa Mbao U- 20, Ismail Mrisho Halfan akipandishwa kwenye gari la Zimamoto baada ya kutokuwepo gari la kubebea wagonjwa kwenye uwanja Kaitaba mjini Bukoba

Gari la zimamoto likiondoka uwanjani Kaitaba ikiwa imebeba mchezaji Ismail kuelekea hospitali ya Mkoa wa Kagera. 
Hivi ndivyo mtanange ulivyokuwa Uwanjani Kaitaba jana jioni

Ismail Mrisho Khalfan ndiye aliyeifungia bao la kwanza Mbao FC. Na hapa akishangilia bao lake la kwanza kwa aina yake kwa Timu ya Mbao Fc.
Ismail Mrisho Khalfan(kulia)
Ismail Mrisho Khalfan(kulia) akitupia shangwe kwenye Camera yetu
Vijana wa Mbao Fc walianza kipindi cha kwanza wakiwa kwenye hali ya kutaka kuibuka na ushindi
Ismail Mrisho Khalfan(kulia) akimkacha mchezaji wa Mwadui fc

No comments

Powered by Blogger.