Header Ads

LIGI KUU VODACOM KUTIMUA VUMBI DESEMBA 17, SIMBA NA YANGA FEBRUARI 18


Na Zainab Nyamka.
LIGI kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena kwa duru la pili kuanzia Desemba 17, huku timu zikishauriwa kukamilisha usajili kwa wakati huku Yanga na Simba kuumana Februari 18 2017..

Dirisha la usajili lililofunguliwa Novemba 15 linatarajiwa kufungwa Desemba 15 na timu zote zimepewa mwongozo wa kutumia mfumo  ule ule wa kutumia mtandao katika kuwasilisha majina hayo usiku wa Desemba 15.

Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Alfred Lucas amesema kuwa ligi inatarajiwa kuanza Desemba 17 kwa mechi nne kuchezwa kwenye viwanja tofauti nchini.

Lucas amesema kuwa kwa sasa ratiba hii imezingatia kalenda ya michezo ya kimataifa, kombe la mapinduzi na kombe la Shirikisho ilihali hawajaweza kuweka ratiba ya michezo ya kimataifa kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo kwani ratiba ya Shirikisho la Mpira Afrika bado hawajaweka ratiba wazi.

Katika ratiba hiyo, Kikosi cha Simba kitaanzia ugenini kuvaana  na Ndanda huku mabingwa watetezi Yanga wakiwa Uwanja wa Taifa kuumana na JKT Ruvu na Azam watakuwa ugenini dhidi ya African Lyon.

No comments

Powered by Blogger.