Header Ads

Kuzaa kwa upasuaji kunaokoa maisha?

Njiya ya upasuaji wakati wa kujifungua mtoto inasaidia kuokoa maishaWanasayansi duniani wanasema kujifungua mtoto kwa njiya ya upasuaji kunaimarisha maumbile, utafiti huu umendiktwa katika jarida la Taasisi ya National Academy of Sciences
Wanawake wengi duniani  wanajifungua watoto kwa njia ya upasuaji kwa sababu njia ya kizazi ni nyembamba.
Kabla ya njia  hii ya upasuaji  kuanza, wanawake wengi walifariki dunia wakati wa kujifungua.
Wanasayansi kutoka Austria wanasema vifo vya wanawake wengi vimepungua wakati wa   kujifungua  kwa sababu ya upasuaji.
Hata hivyo wamegundua pia  mwanamke aliye na njia nyembamba ya kizazi huenda pia mwanawe wa kike akarithi kutoka kwa mama yake.
Watafiti wanasema vifo vya watoto kushindwa kuzaliwa kwa njia ya kawaida vimeongezeka kwa kati ya asili mia 10 na 20.

No comments

Powered by Blogger.