Header Ads

JOH MAKINI NDIO RAPPER ANAEONGOZA KUFANYA KAZI NA WAKALI WA R&B HAPA BONGO


14677234_1778515885735369_4096863772012969984_n


NA JOHN SIMWANZA 

Uhusiano wa Rappers na wasanii wa RnB huwa unatengeneza historia kubwa sana katika kazi zao japo sio kwamba  RnB ikikosekana kwenye  Muziki wa Rap kazi haitokua nzuri lakini  unapochanganya ladha huwa kuna vitu vingi kwenye muziki vinatokaea.

Tuna orodha ndefu sana ya wasanii wanaofanya RnB na Rap hapa Tanzania na kila siku huwa kunakua na ongezeko la wasanii wapya katika kila pande hii inasaidia kuwapa changamoto wasanii waliokuepo wakaze buti na kwa namna moja au nyingie ongezeko la wasanii husaudia  kukua kwa muziki wetu.

Joh makini yupo katika A list ya Rappers wakali wanaoiwakilisha vyema Tanzania katika muziki wa Rap ambao mafanikio yake niya taratibu sana ukilinganisha na muziki wa kuimba hiyo list nikwa mujibu wa kituo cha Mtv kilichopo nchini Afrika kusini na joh makini akiwa anashika nafasi ya Pili katika list hiyo iliyo sheheni wakali wanaosumbua kwa sasa hapa Bongo.


weusi1 (1)

Mwamba Amekua karibu sana na wasanii wa RnB takribani wote wanao ishikilia aina hii ya muziki kwa hapa Tanzania na ukaribu wao mara nyingi umekua ukileta histori kubwa za kazi bila kujali kashirikishwa au kashirikisha sina budi kusema kuwa joh makini ni mpenzi mzuri sana wa RnB ya nyumbani na pengine huenda kama sio kufanya Rap basi joh makini angekua ni miongoni mwa wasanii wa RnB nchini na ndio mana Mwamba wa kaskazini amekutana na wasanii wa RnB mara kwa mara katika nyakati tofauti tofauti na kufanikiwa kuzalisha muziki mzuri.hizi ni kazi alizofanya na wasanii wakali wa RnB Nchini.

     SITORUDI YA Q JAY
Q jay ni miongoni mwa waasisi wa kundi la Wakali kwanza kundi ambalo linasimuliwa mpaka leo na wengi wanatamani lirudi kwakuwa wasanii wote waliokua wakiunda kundi hilo bado wapo.Q jay amesha fanya hit kadhaa kwa wakati ule na alikutana na mwamba wa kasikazini katika ngoma yake ya Sitorudi iliyokuwa ni miongoni mwa nyimbo  kubwa sana Kwa wakati ule na ilifanya vizuri katika chat mbali mbali za radio.

     UNANICHORA YA BEN POL
Ben pol anahistoria kubwa sana katika mziki huu na anaheshima ya tuzo ya mwanamuziki  Bora wa RnB na wakati huo huo joh makini nae ana tuzo ya msanii bora wa hip hop nchini.Wakali hawa walikutana booth na ben pol akampa shavu hit maker huyo wa Perfect Combo kuonesha uwezo wake katika wimbo wa unanichora ngoma iliopokelewa kwa mikono miwili na kuzidi kumpa heshima joh makini kuwa ni miongoni mwa  rapper anaezimiwa sana na wasanii wa RnB.

Johmakini.1

    PENZI YA DAMIAN SOUL
Damian soul amekua yupo karibu sana na joh makini na mara kadhaa wamekuwa wakipeana Support katika kazi zao wanazo zifanya hiyo ni kabla na baada ya kufanya wimbo wa penzi ulio mtambulisha vizuri damiani na kuwaaminisha mashabiki wake juu ya kipawa cha uimbaji alicho Jaliwa.

VITAMINI MUZIKI YA BELLE9
Belle 9 mkali kutoka morogoro nae anaingia katika list ya wasanii wa RnB walio fanya ngoma na joh makini Belle amempa shavu joh katika wimbo wa Vitamini muziki  wimbo uliozua maswali mengi kwa Belle 9 hasa kwa ubunifu alioufikilia na kuteka hisia za mashabiki wake  kingine kikubwa kilichotokea baada ya wimbo huu kutoka ni ikawa ndio jina la Album ya belle 9 ambayo mpaka sas Bado haijatoka.

LOOKING FOR YOU YA JUX
Jux ni miongoni mwa wasanii wa RnB waliopo juu kwa sasa na kadri siku zinavyozidi  jux uwezo wake unazidi kuimarika Lookingi for you ni wimbo ambao alifanya na joh makini na kupelekea kuingia katika listi ya wasanii wa RnB waliofanya ngoma na Rapper huuyu kutoka kaskazini anae wavutia wasanii wengi kufanya nae kazi kwa sasa..

      SINA TIME YA RAMA DEE
Uhusiano wa rama dee na joh makini ni wamuda mrefu sana na umefanikiwa kudumu mpaka sasa na ukaribu huu ulipelekea Kuibariki Good boy ngoma ya Nikki wa pili iliyomtambulisha vizuri kwenye game hii ya muziki wa kizazi kipya rama dee aliudhihilisha ukaribu wake na joh makini kuwa sio tu wa kawaida baada ya kuachia Ngoma ya sina time ngoma ambayo kiukweli iliwashangaza wengi kama ujuavyo RnB ikichanganywa na hip hop sina time ili bamba na kukamatia chati mbali mbali za radio kwa wakati huo.

Joh makini ambae kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Perfect Combo  amekua ni msanii wa rap mwenye mafanikio na muziki wake licha ya kuwepo na kasumba ya hip hop haiuzi lakini joh makini amekua ni mfano bora sana kwa wasanii wanao rap na hivyo tutegemee makubwa sana kwa Joh makini  sababu amesha fanya nyimbo na wasanii wakubwa Afrika akiwemo Davido na Khuli chana Rapper kutoka South Afrika

No comments

Powered by Blogger.