Header Ads

HABARI MPYA: Salama J ndio HOST wa East Africa TV Awards 2016

Na Henry Mdimu
Mtangazaji machachari wa vipindi vya TV aliyevunja rekodi katika ukosoaji uliotukuka, Salama Jabir ametajwa kuta ndiye atakayeendesha tunzo za EATV Jumamosi ijayo zitakazofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.

Roy Mbowe, Mratibu Mkuu wa tunzo hizo amable pia ni mkuu wa Masoko wa EATV amemtaja mwanadada huyo jana usiku saa nne kwamba ndiye atakayekuwa Mc kwa masaa matatu mfululizo akiongoza shughuli hiyo ambayo itarushwa live na kituo cha EATV pekee.

Jumla ya tunzo tisa zitatolewa kwa wasanii wa muziki na filamuwaliofanya vyema kwenye tasnia hiyo huku tunzo moja ya heshima ikitolewa kwamdau mwenye mchango uliotukuka katika tasnia ya sanaa kwa mwaka 2015/16.


Powered by Blogger.