Header Ads

DARK MASTER: Mnapomuenzi Mangwea, mkumbukeni na Mama yake

Na John Simwanza
Mwana chemba Athumani Kabongo a.k.a Dark Master ametoa ya moyoni juu ya wasanii na wadau wanaoandaa show kwa ajiri ya kumuenzi Albert mangwea.

Dark master amesema kuwa kumuenzi mangwea ni kitu kizuri sana kiasi kwamba hata yeye mwenyewe anafurahishwa kuona bado  memba mwenzake anaishi katika mioyo ya watu.

Pia mwanachemba huyo aliongeza kuwa wanapo andaa show bila kutokumshirikisha mzazi wake mangwea inaonesha wazi kuwa wanalitumia jina la mangwea kwa ajiri ya kujipatia vipato vyao binafsi.

"Sipendezwi kabisa na msanii au mdau yoyote atakae andaa show kwa jina la mangwea arafu akashindwa kumshirikisha mzazi wake  au kutokumpatia chochote kilichopatikana  katika show hiyo hapo itakuwa wanalitumia jina la mangwea kwa maslahi yao wenyewe na ndio jambo linaloniuma sana nikisikia hivyo"

Dark Master kwa sasa yupo mkoani Dodoma ambako ndio chimbuko la kundi hili la chemba squard lililo wapoteza wasanii wawili mpaka sasa Mangwea na Mez B na kubaki wawili Ambao ni Norah na Dark master.

No comments

Powered by Blogger.