Header Ads

Ugonjwa wazidisha mapenzi ya Kim kwa Kanye

kim-kardashian-na-kanye-west
 Licha ya rapa Kanye West kuwa katika uangalizi maalumu wa afya yake baada ya kuonekana kuchanganyikiwa, mke wake Kim Kardashian ameonekana kutumia nafasi hiyo kuonyesha mapenzi ya kweli kwa mume wake katika kipindi hiki ambacho anamwuguza akiwa hospitalini..

Mtandao wa Us Weekly umeripoti kuwa Kim ndiye mtu ambaye anaonekana kuwa karibu zaidi kwa Kanye katika kipindi hiki ana amekuwa akishinda hospitali ambayo Kanye amelezwa kwa ajili ya kumfariji mume wake.

Mtu mmoja wa karibu na Kim alisema pamoja na Kim kumfariji Kanye pia amekuwa akilimlisha chakula na hata kulala nae ili tu amsaidie mume wake huyo ambaye walifunga ndoa mwaka 2014 kurudi katika hali yake ya awali.

Kim ni wa tofauti sana,” alisema mtu huo na kuongeza “Anajua sio rahisi kurudi [Kanye] katika hali aliyokuwa nayo awali, amekuwa upande wake katika kila jambo, anamlisha chakula na kulala pembeni yake.”

Kanye West alifikishwa katika kituo cha afya cha Ronald Reagan UCLA, Los Angeles siku ya Jumatatu ya Novemba, 21 baada ya kuonekana kuonyesha hali tofauti ya kuchanganyikiwa wakati akifanya mazoezi nyumbani kwake.

No comments

Powered by Blogger.