Header Ads

Trump amchagua mkosoaji wake mkubwa katika UN

Nikki Haley alikuwa mkosoaji mkubwa wa Donald Trump wakati wa kampeni yake

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemchagua gavana wa Carolina kusini, Nikki Haley, kuwa balozi mpya wa Marekani katika Umoja wa Mataifa.

Kwa njia ya taarifa, amesema kwamba, amethibitisha bayana nia yake ya kuwaleta watu pamoja.

Hiyo imekuwa mojawepo ya nafasi ya juu zaidi katika utawala wake mpya, kumuendea mwanamke au mtu asiye mweupe.

Nikki Haley ambaye alimpinga Trump, wakati wa kampeini za kuwania kiti cha Urais ni Mwamerika wa pili mwenye asili ya Ki-ashia, kuchukua wadhfa wa Ugavana nchini Marekani.

chanzo:bbc

No comments

Powered by Blogger.