Header Ads

PICHA:kuhusiana na moto mkubwa unaoendelea kuwaka Israel

 Moto Haifa, Israel, Alhamisi, Nov 24, 2016Moto mkubwa ambao umekuwa ukiwaka kwa siku kadha Israel sasa unakaribia mji waHaifa  kaskazini mwa nchi hiyo. Moto huo umesababisha uharibifu mkubwa. Watu karibu 50,000 katika mitaa minane wametakiwa kuhama.
Fire fighters work in Haifa, Israel, Thursday, Nov 24, 2016 Wazimamoto wanaendelea na juhudi za kukabiliana na moto huo, ingawa umeathiri maeneo makubwa na wazimamoto hao ni wachache. Wanahitajika pia kuwalinda raia na nyumba zisishike moto.
Haifa, Israel, Alhamisi, Nov 24, 2016   Maelfu ya watu wamehama makwao Haifa, wakijaribu kunusuru mali yao.
 Haifa, Israel, Alhamisi, Nov 24, 2016
 Hakuna taarifa zozote za watu kuumia vibaya lakini watu kadha wamepelekwa hospitalini wakikabiliwa na matatizo kutokana na kupumua hewa iliyojaa moshi.
 Haifa, Israel, Alhamisi, Nov 24, 2016
Miti ikiteketea viungani mwa mji wa Haifa Ukosefu wa unyevu kwenye hewa pamoja na kuwepo kwa upepo mkali kumesababisha moto huo kuenea upesi. 
 Ndege ya jeshi la Israel ikijaribu kuzima moto karibu na Kibbutz Neve Ilan, kaskazini magharibi mwa Jerusalem, Novemba 24, 2016

No comments

Powered by Blogger.