Header Ads

Mtangazaji wa televishioni ya KTN akamatwa Uganda


Tokeo la picha la picha za doren biira

 Mwandishi wa wahabari wa  televisheni ya KTN  kutoka  nchini  Kenya Joy Doreen Biira alikamatwa na kuzuiliwa na polisi wa usalama nchini Uganda usiku wa Jumapili. 

 Vyombo vya habari vinasema Bi Biira alikamatwa pamoja na wengine watano kwa tuhuma za kupiga picha na video kuhusu operesheni ya maafisa  usalama katika kasri la mfalme wa Rwenzururu na kuzichapisha kwenye mitandao ya kijamii.
 
 Waandishi wa habari na mashirika ya kutetea haki za  binadamu wametoa wito kwa serikali kumwachilia huru. wakiwa na hastag #FreeJoyDoreen (Mwachilie huru Doreen) kinachosambaa kwenye  mtandao wa Twitter nchini Kenya. Wanajeshi na polisi walivamia kasri  la Mfalme Charles Wesley Mumbere Jumapili.

 Walinzi wake 46 waliuawa kwa mujibu wa polisi, na wengine 139 walikamatwa. Mfalme huyo alikamatwa pia na kuzuiliwa makao makuu ya polisi ya wilaya ya Kasese kabla ya kupelekwa mjini Kampala. 

 Gazeti la  Monitor nchini uganda limesema mfalme huyo anatarajiwa kukutana na Rais Yoweri Museveni baadae leo.

No comments

Powered by Blogger.