Header Ads

Kompany apata jeraha


 Kompany
 Vincent Kompany ameshiriki mechi tano msimu huu 

Nahodha wa Manchester City Vincent Kompany atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne mpaka  sita kutokana na jeraha la goti,meneja Pep Guardiola amesema.
Mbeligiji huyo alitolewa uwanjani siku ya Jumamosi walipokuwa wakicheza  dhidi ya Crystal palace.
Manchester City walipata ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wa Selhurst.
Kompany mwenye umri wa miaka 30, amefanyiwa uchunguzi na Dkt Ramon Cugat huko Barcelona, na pia daktari wa timu yake ya Manchester City.

''Dkt Cugat amesema  kile ambacho daktari wa klabu hiyo alichosema. Atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne hadi sita ,'' amesema Guardiola.
Kompany ameshiriki kwenye  kikosi cha kwanza katika mechi mbili za ligi msimu huu, na amepata jeraha la mguu na paja mwaka 2016. 

Changamoto yake ya hivi karibuni, ni jeraha lake la 35 tangu kujiunga kwake na Manchester City kutoka kwa klabu ya Ujerumani ya Hamburg mwaka 2008.

No comments

Powered by Blogger.