Header Ads

BENKI YA UBA YATOA MSAADA PUGU SEKONDARI

 Wanafunzi wa Pugu sekondari wakishusha kwenye gari vifaa vilivyokabidhiwa na benki ya UBA kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.
 Mkurugenzi mkuu wa Benki ya UBA,Piter Makao akiwa na meneja operesheni Omary wakikabidhi mafuta ya ngozi kwa kijana mwenye ulemavu wa ngozi ,Daudi Nyangusi na Meneja ufadhili wa elimu kutoka TEA , Tito Mganwa.
 Mkurugenzi mkuu wa Benki ya UBA,Piter Makao akiwa na meneja operesheni Omary wakikabidhi vitabu kwa wanafunzi Salum Mohamed na Ramadhani Juma pamoja na Meneja ufadhili wa elimu kutoka TEA , Tito Mganwa.
 Wafanyakazi waUnited Bank of Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wenye ulemavu wa shule ya Sekondari ya wavulana pugu jijini Dar es Salaam.
 Afisa masoko wa UBA , Evance Chandarua akimkabidhi begi, Ramadahani Juma.

Na  Humphrey Shao.

Benki ya United Bank of Africa(UBA), leo imetoa viti, Magodoro,Magongo ya kutembelea na vitabu vya kujisomea kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya shule ya sekondari ya wavulana Pugu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kutoa vifaa hivyo Meneja wa benki hiyo nchini ,Piter Makao, amesema kuwa wamechagua kutoa vifaa hivyo katika shule hiyo kutokana na mahitaji ya watoto hao ambao wamekuwa wakisoma katika mazingira magumu.
“Vitu hivi ambavyo tumevitoa leo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapunguzia watoto hawa wenye mahitaji maalum kusoma bila  mawazo na kujiona kwamba wao ni sehemu hii ya shule kwa kupata mahitaji yao Yote kama ilivyo kwa wengine”Amesema Makao.

 Ameto  wito kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kufanikiwa katika jamii na baadae wajivunie kuwa walisoma pugu.
Wanafaunzi wenye ulemavu wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya bwalo la shule hiyo.

No comments

Powered by Blogger.