Header Ads

JIONEE: Kili Music Tour ilivyomaliza ngwe yake ya kwanza kwa mbwembwe huko Iringa

Ngwe ya kwanza ya ziara ya kimuziki inayodhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania chini ya udhamini wa bia ya Kilimanjaro imeisha kwa kishindo juzi mkoani Iringa ambapo jumla ya wasanii 10 walipanda jukwaani na kufanya onesho la masaa nane na kukata kiu ya mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo.

Onesho hilo ambalo lilianza saa moja kamili na kuisha saa nane na dakika tano usiku lilikuwa na msisimmko wa aina yake ukilinganisha na maonesho ya mikoa mingine  hasa kutokana na hali ya hewa ya baridi ambayo ilikuwa ikitoa hamasa kwa kila mtu kuangalia huku akicheza kuanzia mwanzo wa tamasha hadi mwisho.

Iringa ni mkoa wa tano kufanyika tamasha hilo ambalo lilianzia mkoani Moshi, kisha likaenda Mwanza, Kahama na Songea na ni mkoa ambao ngwe ya kwanza ya matamasha hayo inaishia kuupisha mwezi mtukufu wa Ramadhan, ambapo ziara hiyo maarufu itaanza tena kutimua vumbi Agosti 9 mwaka huu.

Wasanii waliofunga ngwe hiyo ya kwanza ni pamoja na Snura, Linex, Rich Mavoko, Mwasiti, Izzo B, AY, MwanaFA, Profesa Jay, Weusi, na Juma Nature.

Ukilinganisha na maonesho yaliyotangulia, onesho la Iringa lilikuwa ni la muda mrefu kuliko yote ambapo kila msanii alitumia zaidi ya dakika 45 jukwaani, huku Juma Nature akifunga tamasha na akiwa anapanda kwa mara ya kwanza kwenye matamasha ya ziara hiyo kwa mwaka huu na kupokelewa kwa shangwe kubwa na mashabiki.

Ukiachana na Juma Nature msanii mwingine ambaye ni mara yake ya kwanza kupanda jukwaani kwa msimu huu alikuwa ni Snura ambaye alifungua burudani na pia kupokelewa kwa shangwe na mashabiki kutokana na aina ya muziki anaoufanya. 

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema ziara hii imekuwa na mafanikio makubwa na malengo yametimiwa kwa kiasi kikubwa.

“Tunawashukuru wasanii wote kwa ushirikiano mkubwa na pia mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi katika mikoa yote tuliyoenda…tunawaomba mashabiki wa mikoa iliyobaki wajitokeze kwa wingi,” alisema.

Ziara hii inaratibiwa na kampuni za EATV na East Afrika Radio, Executive Solutions, Integrated Communications, Aggrey & Clifford na AIM Group.

Msimu wa pili wa ziara ya kimuziki ya Kili utaanzia  Mbeya (Agosti 9), Dodoma (Agosti 16), Kigoma (Agosti 23), Mtwara (Agosti 30)  na onesho kubwa la hitimisho litafanyika Dar es Salaam Septemba 6
PICHANI JUU: 
Msanii mkongwe Profesa J akifanya vitu vyake wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa CCM Samora Jumamosi Juni 21, 2014. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rich Mavoko na wachezaji wake wakifanya show ya aina yake  wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa CCM Samora Jumamosi Juni 21, 2014. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii Snura akifanya vitu vyake pamoja na madansa wake wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa CCM Samora Jumamosi Juni 21, 2014. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Maelfu ya mashabiki waliojitokeza wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa CCM Samora Jumamosi Juni 21, 2014. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii maarufu wa Bongo flava, Juma Nature akitoa burudani wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa CCM Samora Jumamosi Juni 21, 2014. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii maarufu, Linex akipagawisha wakazi wa Iringa wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa CCM Samora Jumamosi Juni 21, 2014. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mwasiti akicheza na mmoja wa mashabiki wake wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa CCM Samora Jumamosi Juni 21, 2014. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Wasanii wa hip hop wanaounda kundi la Weusi, Joh Makini na Nick wa Pili wakifanya onesho la aina yake wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa CCM Samora Jumamosi Juni 21, 2014. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii machachari wa muziki wa kizazi kipya toka mkoani Mbeya, Izzo B akiwapa kitu roho inapenda  wakazi wa mji wa Iringa katika Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa CCM Samora Jumamosi Juni 21, 2014. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Wanamuziki  Mwana FA na AY wakionesha ishara ya kumalizika kwa ngwe ya kwanza ya tamasha la Kili Music Tour lililofanyika katika Uwanja wa CCM Samora. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

No comments

Powered by Blogger.