Header Ads

PICHA: Viongozi wa dini warejea kutoka Thailand walikoenda kujifunza kuhusu gesi

 Baadhi ya viongozi wa dini kutoka katika Mikoa ya Lindi na Mtwara wakiwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) kutokea nchini Thailand. Viongozi  hao walifanya ziara nchini humo kwa ajili ya kujifunza na kupata uzoefu wa uendelezaji wa sekta ya gesi.
Viongozi wa dini  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) kutokea nchini Thailand.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Baraza la Waislamu  Tanzania (BAKWATA) Bw. Mohamed Sinani akielezea jinsi nchi ya Thailand ilivyopiga hatua kimaendeleo kutokana na mchango wa sekta ya gesi
 Padri Dkt. Aidan Msafiri ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino tawi la Mtwara akizungumza na waandishi wa habari  katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) mara baada ya kuwasili kutoka nchini Thailand.
 Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania kutoka dayosisi ya Newala Bw. Oscar Stephen akizungumza  kwa niaba ya viongozi wenzake uzoefu walioupata walipokuwa nchini Thailand hususan katika sekta ya gesi.
 Shehe Mkuu kutoka Mkoa wa Mtwara Bw. Nurdin  Abdalah akiwaeleza waandishi wa habari jinsi  wananchi wa Thailand walivyoweza kutunza vyema rasilimali yao ya gesi ikiwa ni pamoja na usimamizi wa sekta nyingine.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Abdallah Hamis Ulega akizungumza na waandishi wa habari jinsi wananchi wa  Thailand walivyonufaika na rasilimali ya gesi.

No comments

Powered by Blogger.