Header Ads

Airtel Yazindua LUKU OFA kupitia huduma ya Airtel Money

Dar es Salaam, Mei 5th 2014 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua ofa mpya itakayowawezesha wateja wake kupata LUKU Bonus kila wakati watakaponunua LUKU kupita huduma Airtel Money, ofa ambayo ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel katika kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora nchini.

 Akiongea kuhusu ofaa hii Meneja wa kitengo cha Airtel Money Asupya Naligingwa(Pichani yojuu) alisema ofa hii imelenga katika kuwawezesha wateja kutumia huduma ya Airtel Money kununua Luku  kwa urahisi, usalama na  haraka zaidi.  

"Wateja wetu watapata LUKU unit s bonus zao hapohapo pale watakaponunua luku kwa kupitia huduma ya Airtel Money, Bonus hii wataipata mara nyingi kwa kadri watakavyonunua LUKU kwa siku. Ofa hii inaendana na ulimwengu wa maisha ya kisasa kwani inaokoa muda na kurahisha kufanya manunuzi kwa urahisi mahali popote na wakati wowote".

"Natoa wito kwa wale ambao hawajawahi kutumia huduma hii wafanye sasa kwani tuanishi katika ulimwengu ambao kutunza muda ni muhimu sana”

Nalingigwa aliongeza kwa kusema huduma hii ni kwa wateja wote wa Airtel nchi nzima  hakuna haja ya kujiunga au gharama yoyote kutozwa ili kufurahia  Bonus kwa manunuzi ya LUKU kupitia huduma ya Airtel Money

“ili kupata huduma ya Airtel Money mteja anatakiwa kupiga *150*60#  na kuunganishawa na orodha ya Airtel Money itakayokuwezesha kufanya miamala mbalimbali ikiwemo kununua LUKU

Airtel Tanzania inatoa huduma ya fedha kwa njia ya huduma ya Airtel Money ambapo imekuwa msaada mkubwa katika maisha ya watanzania.  Jitihada  za kuwezesha upatikanaji wa huduma za Airtel Money nchini umeendelea kuwa wa mafanikia  ambapo imeweza kuwa na mawakala wa Airtel Monye zaidi ya 35,000 nchi nzima na kuwezesha upatikanaji wa huduma za kifedha na manunuzi ya bidhaa mbalimbali kuwa rahisis na ufanisi zaidi. 

Huduma hii imekuja kwa wakati muafaka hivyo napenda kuwahamasisha wateja kuendelea kufurahia huduma hii ya Airtel Money”.aliongeza Naligingwa

Huduma ya Airtel Money inawawezesha wateja wake kufanya malipo ya ankra za bidhaa na huduma kama vile . DAWASCO, LUKU, USA visa, DSTV,  pamoja na kununua muda wa maongezi, kununua vifurushi vya yatosha , kutuma na kupokea  pesa kwa nusu gharama na Bure kupitia vifurushi vya bure pack  pamoja na huduma nyingine nyingi

No comments

Powered by Blogger.