Header Ads

WTF? ...Utata kwenye Tangazo la Airtel lenye picha ya Wema

Wakati Superstar Wema sepetu akianza kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye matangazo ya simu za mkononi kupitia kampuni ya simu ya Airtel ambayo leo imetangaza kuwapa uhondo wa kuperuzi mitandao ya kijamii bure, herufi tatu zilizoandikwa kuainisha mitandao mitatu ya kijamii kwa kifupi zimezua utata mtandaoni.

Mjadala mkubwa upo katika mtandao wa Twitter ambapo watu mbali mbali wakihoji uhalali wa kuweka herufi WTF, ilhali herufi hizo pia humaanisha neno jingine ambalo si la kimaadili?

Katika tangazo hilo kampuni hiyo ya simu imetangaza kutoa bure huduma ya Ahatsaap, Twitter na Facebook ambapo ukiziunganisha zote, unaweza kusema WTF bure!

No comments

Powered by Blogger.