Header Ads

Washindi wa droo ya tisa ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti watajwa Wiki iliyopita tumeshuhudia mshindi wa pili wa tiketi ya kwenda Brazil Bw Menrald Shayo akijinyakulia tiketi yake katika droo ya 8 ya “winda safari ya Brazil na Serengeti”. Pamoja na tiketi hiyo pia kulikuwa na washindi wawili wa simu aina ya Samsung tablet na washindi watano wa ving’amuzi. 

Mapema leo kampuni ya bia ya Serengeti imechezesha droo yake ya 9 ambapo washindi wawili Chifu John Nyanda mstaafu kutoka Mororgoro na Bw Michael Solomon Laizer mstaafu kutoka Dar es Salaam Wameibuka washindi wa simu aina Samsung galaxy tab. 

Droo hii ilichezeshwa leo asubuhi katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti huku ikishuhudiwa na waandishi wa habari, maofisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, PWC na push mobile media. Promosheni hii bdo ina wiki 4 hadi kufika mwisho na droo kubwa 1 za kujishindia tiketi za kwenda Brazil.

Mshindi wa kwanza wa simu aliongea kwa furaha baada ya kupewa taharifa za ushindi huo kwa njia ya simu na Meneja wa bia ya Serengeti, Bw Michael Laizer alisema kuwa hakutegemea kupata zawadi hizi na kwake imekuwa ni zawadi kubwa toka bia ya Serengeti. Aliishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kujali wateja wake na kuwapa zawadi mbalimbali.

Nae mshindi wa pili Chifu Nyanda alisema kuwa amefurahia sana kupata zawadi ya simu ya kisasa ambayo hakuitegemea, katika mazungumzo hayo kwa njia ya simu aliwashauri wateja wa Serengeti kushiriki promosheni hiyo kwa sababu ni ya ukweli na zawadi zipo kweli, aliishukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa zawadi yake na kuahidi kuendelea kushiriki mpaka apate tiketi ya kwenda Brazil.

Washindi watatu waliojishindia zawadi katika droo ya 8 ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti pia walikabidhiwa zawadi zao. Washindi hao ni Bruno Thobias Muhangwa aliyejipatia simu ya kisasa aina ya Samsung tablet na wengine ni Alex Vincent na Henry Martin waliyejishindia ving’amuzi. Washindi hao waliishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwajali na kuwaweka mbele wateja wao kwa kuja na ofa mbalimbali zinazomnufaisha mteja wao.

 Nae Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo alisema kuwa promosheni hii ipo wazi kwa wanywaji wote wa bia ya Serengeti, na mpaka sasa kumekuwa na washindi Zaidi ya 200000 waliojishindia bia za bure na pia zaidi ya washindi 30000 wa fedha taslimu kiasi cha shilingi 5000 na 10,000. Alisema “promosheni ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti bado inaendelea.

PICHANI JUU: Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo(wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa droo ya nane ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao mapema leo katika Kiwanda cha Bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam kutoka kushoto Henry Martin, Bruno Thobias na Alex Vicent(wa kwanza kulia) ambao wamejipatia ving’amuzi na simu aina ya Samsung Galaxy Tablet.
 Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo(kushoto) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tisa ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti wakati wa droo ya tisa iliyofanyika mapema leo jijini Dar es Salaam, anayemshuhudia ni Afisa Mwandamizi kutoka PWC Golder Kamuzora.
Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo(wa pili kulia) akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wana habari mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya nane ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti mapema leo katika Kiwanda cha Bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam kutoka kushoto ni Bruno Thobias,  Henry Martin na Alex Vicent (wa kwanza kulia).


No comments

Powered by Blogger.