Header Ads

PICHA: Uzinduzi wa Zanzibarlicious na ilivyodhamiriakukomboa wanawake

DSC_0271
Na Zainul Mzige, Zanzibar.
UMOJA wa Wanawake wa Zanzibarlicious umeamua kuwakomboa wanawake kutoka katika utumwa wa kiuchumi kwa kuwawezesha kwa kuwapa ujuzi na maarifa ili kujikwamua kwenye umasikini.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa umoja huo, Umul-kulthum Ansel wakati wa uzinduzi wa umoja huo kwenye sherehe zilizofanyika mwishoni mwa juma katika Hoteli ya Ocean View Beach Resort mjini Unguja.

Alisema lengo la kuwakwamua wanawake ni kutokana na kuonekana wao na watoto ni waathirika wakuu wa mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa yanayoendelea katika maeneo mbalimbali ulimwenguni hasa katika bara la Afrika.

“Umoja huu umeundwa kwa lengo la kuwashajihisha,kuwahamasisha ,kuwaunganisha na kuwaendeleza wanawake kwa kuwapa ujuzi na maarifa ili waweze kujitambua na kuithamini nafasi yao katika kuleta maendeleo,”alisema.

Alisema malengo ya umoja huo ulioanzishwa mwaka 2011 na kusajiliwa mwaka jana ni kumuendeleza na kumuwezesha mwanamke kiuchumi,kijamii na kimwenendo.

Alisema umoja huo umekuwa ukitoa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi vya wanawake na kuwawezesha kubuni biashara ndogondogo na jinsi ya kuweza kutafuta mitaji kutoka taasisi mbalimbali za kitaifa.

“Pia tunatoa ushauri nasaha kwa masuala ya familia, waathirika wa virusi vya Ukimwi na Dawa za Kulevya,”alieleza Mwenyekiti huyo.

 Vilevile Zanzibaliciuos inatoa ushauri wa kisheria katika masuala ya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto pamoja na kuwakutanisha wanawake kutoka sehemu mbalimbali kupitia maonesho ya kibiashara na kwenye sherehe za kitaifa.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mwanaidi Salehe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, alisema masuala ya wanawake yapo chini yake hivyo atahakikisha anawasaidia kwa kila namna.

Katibu Mkuu huyo ambaye alichangia Sh milioni moja kusaidia umoja huo alisisitiza kuwa “lazima tuzipiganie haki zetu wanawake, tuelimishane na tupendane na tuanze kwa watoto wetu wa kike tuwape mafunzo bora na kuwalinda wasijiingize kwenye vitendo viovu kama kuepuka dawa za Kulevya”.

PICHANI JUU: Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Mwanaidi Salehe akisaini kitabu cha wageni cha Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious kwenye sherehe za uzinduzi wa Umoja huo zilizofanyika mwishoni mwa juma kwenye Hoteli ya Ocean View Beach Resort mjini Unguja.(Picha zote na Zainul Mzige).
DSC_0284
Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious Bi. Evelyne Wilson (wa pili kushoto) akitoa maelezo ya picha na kazi mbalimbali walizofanya kwa jamii mara baada ya kuwasili mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious, Bi. Umul-Kulthum Ansel (Madam Ummy).
DSC_0289
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Mwanaidi Salehe akitizama picha mbalimbali zinazoonyesha kazi walizofanya Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious kwa jamii inayowazunguka visiwani humo.
DSC_0302
Wageni waalikwa wakiipokea meza kuu.
DSC_0311
Meza kuu katika nafasi yao kutoka kushoto ni Mkurugenzi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa FAWE, Bi. Khadija Ally Mohamed, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious, Bi. Umul-Kulthum Ansel (Madam Ummy), mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Mwanaidi Salehe pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Uwezeshaji, Bi. Fatma Gharib Bilal.
DSC_0318
Mshehereshaji kwenye uzinduzi wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious, Bi. Fauziat Abood.
DSC_0360
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious, Bi. Umul-Kulthum Ansel (Madam Ummy), akisoma risala yake mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa (hawapo pichani).
DSC_0379
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Mwanaidi Salehe akitoa baraka zake kwenye uzinduzi wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious mjini Unguja.
DSC_0371
Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious Bi. Evelyne Wilson akiteta jambo na mjumbe wa Umoja huo Bi. Sheha Hilal.
DSC_0323
Pichani juu na chini Baadhi ya Wanawake wanaounda Umoja wa Zanzibalicious na wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mwenyekiti wa Umoja huo kwenye sherehe za uzinduzi wa kukata na shoka uliofanyika kwenye hoteli ya Ocean View Beach Resort mjini Unguja.
DSC_0393
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Mwanaidi Salehe, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious mjini Unguja.
DSC_0002
Cake maalum katika kusheherekea uzinduzi wa Zanzibalicious Women Group.
DSC_0405
Mgeni rasmi Bi. Mwanaidi Salehe akikata cake maalum iliyoandaliwa kusindikiza uzinduzi wa Umoja huo.
DSC_0410
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious, Bi. Umul-Kulthum Ansel (Madam Ummy), akimlisha kipande cha cake mgeni rasmi kama ishara ya kumshukuru kwa kushiriki nao katika uzinduzi wa Umoja huo.
DSC_0417
Mgeni rasmi Bi. Mwanaidi Salehe akimlisha cake mdau wa masuala ya wanawake Bi. Mariam Abdallah.
DSC_0419
Mshehereshaji Bi. Fauziat Abood akianzisha mnada kwa wageni waalikwa kwa kuuza kipande cha cake kwa shilingi 10,000/= kwa ajili ya kuchangia Umoja huo ambao Wanawake wa Umoja huo wamekuwa wakijichangisha fedha kutoka mfukoni mwao kwa ajili ya kuisadia jamii hususan wanawake na waathirika wa Madawa ya Kulevya.
DSC_0434
Kina baba nao walihamasika kuunga mkono zoezi hilo ambapo walilishwa vipande vya cake na mgeni rasmi Bi. Mwanaidi Salehe.
DSC_0452
Mmoja wa wadhaminiwa sherehe hizo kutoka kampuni ya FAITH Tours and Safaris akilishwa kipande cha cake na mgeni rasmi.
DSC_0456
Burudani kutoka COCONUT BAND ambayo ndio habari ya mujini visiwani Unguja chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wake Bw. Raymond.
DSC_0485
Mshehereshaji Bi. Fauziat Abood akikteta jambo na mwimbaji taarab mkongwe Bi. Zuhura Shaabani.
DSC_0503
Mjumbe wa Umoja na Wanawake wa Zanzibalicious Sheha Hilal na Makamu mwenyekiti wa Umoja huo Evelyne Wilson wakimwaga manoti kwa mwimbaji mkongwe wa taarab mjini Unguja Bi. Zuhura Shaabani alipokuwa akitoa burudani kwa wageni waalikwa kwenye sherehe za uzinduzi wa Umoja huo.
DSC_0588
Uliwaidia ule wasaa wa mahanjumaati yaliyoandaliwa na hoteli ya Ocean View Beach Resort kwa wageni waalikwa.
DSC_0565
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Uwezeshaji Zanzibar, Bi. Fatma Gharib Bilal akiongoza meza kuu kupata Dinner kwenye sherehe za uzinduzi wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious.
DSC_0618
Wageni waalikwa wakijisave msosi wa nguvu, chezea Unguja wewe kwa kukaangiza....!!!
DSC_0631
It's Dinner time... ndani ya hoteli ya Ocean View Beach Resort.
DSC_0641
Mshereshaji Bi. Fauziat Abood akiendesha harambee ya kutunisha mfuko wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicous kwa kunadi vitu mbalimbali kwa wageni waalikwa.
DSC_0660
Makamu Mwemyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious Bi. Evelyne Wilson akizunguka kwenye meza za wageni waliohidhuria sherehe za uzinduzi wa umoja huo kunadi vitu mbalimbali.
DSC_0666
Mnada ukiendelea.
DSC_0672
Hili litamfaa mke wa wangu, zuri.....! Mambo ya LVD mjini Unguja....Baba akionekana kuvutiwa na pochi lililotengenezwa na kitenge wakati wa mnada.
DSC_0680
Madam Ummy nae akinadi T-shirt kwa mdau wa Fisherman Tours.
DSC_0691
Mr. Otembo aalinunua T-shirts hizo kwa Tshs 200,000/= katika kuchangia jitihada za Umoja huo kuwafikia jamii visiwani Unguja.
DSC_0464
Pichani juu na chini wageni waalikwa wakibadilishana mawazo na kufurahi wakati wa sherehe za uzinduzi wa Zanzibalicious Women Group.
DSC_0535
Walipendezaje...!!
DSC_0723
Makamu mwenyekiti akitoa utambulisho wa Wanawake wanaounda Umoja wa Zanzibalicious kwa wageni waalikwa.
DSC_0790
Mgeni rasmi na meza kuu kwenye picha ya pamoja na Zanzibalicious Women Group.

No comments

Powered by Blogger.