Header Ads

MREJESHO: Kuhusu Familia Kitchen Party Galla Tour, na picha za Dodoma wikiendi iliyopitaThe PSI/TZ ni Shirika lisilokuwa la kiserikali lililojikita katika kuboresha maisha ya watanzania  kwa kutoa elimu na huduma za afya pamoja na  kusambaza bidhaa za afya kote nchini. Katika kupambana na magonjwa sugu kama vile UKIMWI, Kansa ya Kizazi, Malaria na haswa vifo vya akina mama, PSI/ Tanzania hushirikiana na wizara ya afya kuhakikisha malengo ya millenia kwa upande wa afya yanatimia.

PSI/ Tanzania iliazisha huduma za afya kupita chapa (Brand)yake ya FAMILIA  mwaka 2010 ikiwa na huduma za uzazi wa mpango na baadae mwaka 2013 huduma ziliongezeka zikiwemo afya ya watoto, huduma za mwanamke baada ya kuharibika kwa mimba na kanza ya kizazi. Familia hufikisha huduma hizi kwa jamii kwa Kupitia wadau wake katika serikali na sekta binafsi za vituo za afya. 

Hivi sasa, Familia inafanya kazi na vituo vya afya binafsi visivyopungua 250 katika mikoa 13 ya Tanzania ikiwemo , Dar es Salaam, Coast, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Mara, Tanga, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Iringa, Mbeya na Arusha

Kampeni hii iliyojikitika katika kutoa elimu  sahihi ya uzazi wa mpango na kansa ya kizazi ,kutoa huduma na hatimaye kupunguza vifo vya kina mama ina makusudi hayo kwa sababu hapa nchini, Kansa ya kizazi  sio tu kansa inayoongoza katika vifo vya kina mama bali pia ni aina ya kansa ambayo imekuwa ikikua kwa kasi na katika nchi hizi za Afrika Mashariki, Tanzania ina  tatizo  kubwa zaidi ya gonjwa hili ikisababisha vifo 37.5 katika ya wanawake 100,000.  

Kwa swala la Uzazi wa mpango, matumizi yake yamekuwa yakikua katika kasi ndogo kwa  sababu ya elimu duni kwa wanajamii na kwa ujumla kukosekana kwa matumizi haya, wanamama wengi hasa vijijini wamekuwa wakizaa mara kwa mara jambo ambalo linawapelekea kuzorota kwa afya zao na pia afya duni za watoto wanaowazaa na hata kupoteza maisha wakati wa uzazi .
 
Katika harakati za kupunguza vifo vya kina mama, Kupitia nembo yake ya Familia, PSI imeshirikiana na Women in Balance kuwaletea  “Familia Kitchen Party Gala Tour” itakayofanyika katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Dar es Salaam. 

Sherehe hizi ambapo hujulikana kuhudhuriwa kwa wingi na kina mama zina kusukudio la ziada la kuhakikisha kuwa pamoja na elimu ya ujasiriamali, saikologia, na kijamii, mwanamke anapata fursa ya kujitambua, Kujipenda na Kujithamini katika swala zima la afya ya uzazi na kansa ya kizazi.  Dhima ya ushirikiano huu ni kwa lengo la;
1.       Kupunguza vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi,
2.       Kutoa elimu sahihi kuhusiana na uzazi wa mpango pamoja na afya ya kizazi,
3.       Kutoa huduma hizi wakati wa Shughuli hii.
Familia imedhamiria kuhakikisha kuwa Mwanamke/Mwanamama wa Dodoma wanapata ufahamu na elimu sahihi pamoja na kutoa mwongozo wa wapi pa kupata huduma hizi za uzazi wa mpango pamoja na upimaji na matimabu ya awali ya kansa ya kizazi.

PICHANI JUU: Mmoja kati ya wajasiriamali akiweka sawa bidhaa zake, katika ukumbi wa Kilimani Dodoma juzi ambapo Familia Kitchen Party Galla ilifanyika
 Hapa ni wajasiriamali zaidi wakiweka sawa bidhaa zao
 Jukwaa lenyewe sasa...
 Red Carpet pia ilikuwepo
 Wamependeza hawajapendeza?
 Burudani matata kutoka kwa shilole iliporomoshwa pia
 Neno kutoka kwa Aunt Sadaka Gandhi, likatoka
 ...na mduara ukapigwa kuleta raha

No comments

Powered by Blogger.