Header Ads

Meya Slaa aanza utekelezaji wa moango wake wa Mayoy's Ball

DSC_0428
Na Zainul Mzige
“Kiongozi hapaswi kutegemea nguvu za Serikali kufanya shughuli za maendeleo” Hayo ni maneno ya  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto, Jerry Silaa katika hafla ya kukabidhi madawati kwa shule tatu za sekondari zilizopo Manispaa ya Ilala iliyofanyika Shule ya sekondari Pugu.

Katika hafla hii, jumla ya madawati 300 yenye thamani ya shilingi milioni 45 za kitanzania yaligawiwa kwa shule 3 zilizopo manispaa ya Ilala ambazo ni Shule ya sekondari Pugu (107), Shule ya sekondari Ulongoni (93) na Shule ya sekondari Jangwani (100) kupitia jitihada zake za kuanzisha mpango wa Mayor’s Ball 2013 ulioanza mwaka jana kupitia kampeni ya “Dawati ni Elimu, Kalisha mmoja, boresha Elimu”.

Bwana Silaa alitoa pongezi na shukrani za dhati kwa wote waliotimiza ahadi zao katika kufanikisha zoezi zima la ununuzi wa madawati mapya na kufanikisha kampeni yenye lengo la kuinua viwango vya elimu ya sekondari na msingi Tanzania. Pia, alichukua nafasi kuwaomba wadau waendelea kujitokeza kuchangia elimu kwani ni mara ya kwanza kwa jambo hili la “Mayor’s Ball” kufanyika nchini.

“naomba nitumie nafasi kuwapongeza wadau wote walioitikia wito huu na naomba kutoa rai kwa wale wote walioahidi kutimiza ahadi zao ili kufanikisha lengo la kampeni hii iliyobeba kauli mbiu ya Dawati ni Elimu kalisha mmoja, boresha elimu”, alisema Mstahiki meya Jerry Silaa.

Katika hotuba yake, amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii hasa baada ya kuwaboreshea mazingira ya kusomea kwa msaada wa madawati mapya na ya kisasa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Imelda Samjela, ameiomba serikali kuu kuiangalia shule ya Sekondari Pugu kwa jicho la pili kutokana na hadhi yake ya kutoa viongozi nchini na kuifanya iwe na hadhi ya kimataifa. Shule ya sekondari Pugu inajivunia sifa ya kuwa shule  iliyozaa viongozi shupavuTanzania akiwemo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bi. Imelda aliongeza kuwa kila mwaka tunapoadhimisha Maisha ya Mwalimu Nyerere basi kufanyike jambo aidha kupaka rangi na kusafisha mazingira ya shule hiyo iliyobeba historia ya Taifa la Tanzania. Diwani pia alitoa wito wa kuweka fungu la fedha za kukarabati majengo ya shule hiyo pamoja na kutokomeza kero ya Kunguni shuleni.

 Kunguni wamekuwa ni kero kubwa kwa wanafunzi hasa wakati wakulala. Alitoa angalizo hili kwa mwenyekiti wa huduma za jamii.

Akitoa ufafanuzi wa suala la ukarabati wa majengo ya shule hiyo, Mwenyekiti wa huduma za Jamii Manispaa ya Ilala, Bi. Angelina Nalembeka amesema kuwa Manispaa ilishatoa shilingi Milioni 50 kwa ajili ya ukarabati na wanampango endelevu wa kufanya hivyo kila mwaka. 

Mpango huu si tu kwa shule ya Pugu bali kwa shule nyingine pia zinazoizunguka manispaa ya Ilala.

Mwenyekiti huyo pia alithibitisha kufanyika kwa zoezi la awali la kutokomeza Kunguni shuleni kwa kunyunyiza dawa na kuwepo kwa mpango endelevu wa kunyunyiza dawa ili kuondoa kabisa kero hiyo ya Kunguni shuleni.

 PICHANI JUU: Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, ambaye pia ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akiwasili kwenye shule ya sekondari Pugu kwa ajili ya kukabidhi madawati 300 kwa shule tatu zilizopo manispaa ya Ilala na kulakiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Jovinus Mutabuzi.(Picha zote na Zainul Mzige).
.
DSC_0431
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa, akisaini kitabu cha wageni katika shule ya sekondari Pugu mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
DSC_0446
Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari Pugu, Jovinus Mutabuzi(mwenye suti nyeusi) akizungumzia changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo mbele ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa. wengine pichani ni wakuu wa shule za sekondari Ulongoni na Jangwani waliojuika katika hafla hiyo ya kukabidhiwa madawati.
DSC_0456
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipitia moja ya mafaili ya taarifa za shule hiyo.
“Mheshimiwa Diwani amefuatilia suala lenu la Pugu kwa umakini na taarifa zake tunazo katika Halmashauri. Mwalimu mkuu atakuwa shahidi na tumeshakuja kupiga dawa na bado mwaka huu tutakuja kupiga dawa tena kuondoa Kunguni” alisema Mwenyekiti, Huduma za Jamii.
Aidha, Mwenyekiti wa huduma za Jamii Manispaa ya Ilala aliongeza kuwa suala ya kero la Maji liko kwenye utatuzi kamati yake ya manispaa yake ilishatembelea shuleni hapo na kuona kero hiyo.
Amempongeza Mstahiki Meya kwa juhudi zake za kutatua tatizo la madawati na ameomba wengine pia ambao ni viongozi wakubwa serikalini waliosoma shuleni hapo wakumbuke walipotoka na kusaidia kuiweka katika hali nzuri.
DSC_0479
Meza kuu ikipokea heshima ya ukaribisho kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Pugu (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Kaimu Diwani wa Upanga Magharibi, Bi. Jokha Lemki, Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela, Mstahiki Meya, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Jovinus Mutabazi na Mwenyekiti wa Hudama za Jamii Manispaa ya Ilala, Angelina Malembeka.
DSC_0490
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Jovinus Mutabuzi akielezea furaha yake ya kupokea madawati 107 yaliyotolewa na mpango wa Mayor's Ball 2013 kupitia kampeni ya "Dawati ni Elimu" chini ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
DSC_0521
Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela, akiwasilisha kero ya shule ya Sekondari Pugu kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kuhusiana na wadudu aina ya Kunguni kwenye mabweni ya wanafunzi shuleni hapo ambapo imekuwa kero kubwa wakati wa kulala na kuwasababisha usumbufu.
DSC_0524
Sehemu ya madawati  kati ya 300 yaliyotolewa na mpango wa Mayor's Ball 2013 kupitia kampeni yake ya "Dawati ni Elimu" inayolenga kutatua uhaba wa madawati kwa shule zilizomo ndani ya Manispaa ya Ilala.
DSC_0546
Mwenyekiti wa huduma za jamii manispaa ya Ilala, Angelina Nyalembeka akitoa ufafanuzi kuhusiana na kero za wadudu aina ya Kunguni katika shule hiyo ambapo amesema mwaka jana walipulizia dawa kwenye mabweni yote ya wanafunzi na haraka iwezekanavyo ataliwasilisha kero hiyo kwenye vikao vya Manispaa na kupatiwa ufumbuzi na wanafunzi waweza kukaa kwa amani bila usumbufu.
DSC_0572
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto, Jerry Silaa, akizungumza na waalimu pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Pugu, kabla ya kukabidhi madawati kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
DSC_0527
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Pugu wakifuatilia risala ya mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa.
DSC_0622
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiteta jambo na mmoja wa wanafunzi wa kidato cha tatu ambaye ni mlemavu Voster Peter wakati akikabidhi madawati shuleni hapo.
DSC_0482
Baadhi ya viongozi wa Kata ya Pugu, Gongo la Mboto na Upanga Magharibi waliohdhuria hafla hiyo.
DSC_0626

No comments

Powered by Blogger.