Header Ads

Jhikoman & Afrikabisa band kuanza Europe Tour mwezi huu April 2014

 
Mkali wa muziki wa Reggae kutoka Afrika Mashariki mwenye makazi yake wilayani bagamoyo, mkoa wa Pwani, Jhiko Manyika(Pichani), marufu kwa jina la Jhikoman, anatarajiwa kuondoka nchini katikati ya mwezi huu
kuanza ziara ya miezi mitatu barani ulaya, ambapo atatumbuiza katika maonyesho makubwa ya kimataifa huko ughaibuni.

Baadhi ya festival zitakazo funikwa na mwanamuziki huyo ni Helsink Film Festival kule Finland, na Norway na imebainika kuwa Jhikoman pia atashirikiana jukwaa na wazee wa kazi FFU Ughaibuni a.k.a "watoto wa mbwa" Ngoma Africa band katika maonyesho makubwa ya Tubingen,Ujerumani yatakayo fanyika kuanzia 17 mpaka 20 Julai 2014.

Hivi karibuni, Jhikoman na bendi yake ya Afrikabisa Band, ametajwa kuwa ni balozi nyota bora ya Reggae anayekubalika kimataifa na anaweza kumudu kutingisha jukwaa lolote kubwa la kimataifa.

No comments

Powered by Blogger.