Header Ads

*'BIG RESULTS NOW' KUFANIKISHA UBIA KATI YA SEKTA BINAFSI NA ZA UMMA

  Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger', iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, hivi karibuni. Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now). Picha na Sufianimafoto.com
******************************
 Na Mwandishi Wetu
Serikali inalenga kushirikiana na sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya kimkakati yenye thamani ya shilingi trioni 6 hadi kufikia mwaka 2015/16 ikiwa ni sehemu ya ukamilishwaji wa mkakati wa “Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa” yaani Big Results Now (BRN), utaratibu unaotumiwa na Serikali katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kwa lengo la kupata matokeo makubwa kwa muda mfupi. 

Katika mkuitano wake na wamiliki wa magazeti tando, msemaji mkuu wa wizara ya Fedha, Bi Ingiahedi Mduma alibainisha kuwa kuna vyanzo vingi vya fedha ambavyo wizara yake imedhamiria kuvitumia lakini kwa hii ambayo wanatarajia kushirikisha sekta binafsi ipo miradi mitatu mikuu ambayo inatarajiwa kutoa muongozo.


Bi mduma aliitaja miradi hiyo ya awali kuanza kutekelezwa kwa ubia ni ujenzi wa barabara ya Dar es Salaam hadi Chalinze, uendeshaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, na ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi III. Amesema ukiachana na miradi hii, Wizara ya Fedha inaendelea kutekeleza jukumu la kutafuta na kutoa fedha za kugharamia shughuli za BRN zilizoibuliwa katika maabara zote sita za Elimu, Maji, Kilimo, Uchukuzi, Nishati na utafutaji na mapato ya serikali.


Bi Mduma ameelezea pia kwamba katika kipindi cha Julai hadi Disemba, 2013 Wizara ya Fedha imefanikiwa kutekeleza kiashiria hiki kwa kutoa fedha za maendeleo za ndani kwenye Wizara zinazotekeleza shughuli za BRN.

Amesema jumla ya shilingi Bilioni 590.5 zimetolewa katika kuhakikisha kwamba maabara hizi zinaweza kujitegemea katika miradi yake.

Akitaja viwango nvya fedha ambavyo wizara imetoa, Bi Mduma alisema miradi ya Elimu imepewa jumla ya shilingi bilioni 8.3, Miradi ya Maji imepewa shilingi bilioni 86.0, Miradi ya Kilimo shilingi bilioni 10.2, Miradi ya Uchukuzi shilingi bilioni 146.6 na Miradi ya Nishati imepewa jumla ya shilingi bilioni 339.4.

No comments

Powered by Blogger.