Header Ads

Matumizi ya gesi kuokoa Trilioni moja kwa mwaka

Serikali imesisitiza kuwa itakuwa ikiokoa zaidi ya shilingi Trilioni Moja kwa mwaka, kutokana na kuachana na matumizi ya mashine za umeme za kukodi, wakati itakaoanza kutumia rasmi umeme unaotokana na gesi mwishoni mwa mwaka huu.

Hatua hiyo imeelezwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Pichani) wakati akihitimisha ziara yake ya siku Mbili iliyolenga kukagua ujenzi wa Miundombinu ya Gesi katika Mikoa ya Mtwara na Kinyerezi jijini Dar es salaam.

Balozi Sefue amesema utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo ni mkakati wa serikali wa Matokeo Makubwa Sasa, hivyo serikali haitavumilia mtu au kampuni itakayokwamisha au kuchelewesha kukamilika kwa mradi huo.

Katika ujenzi wa Mitambo ya Kinyerezi unaotarajiwa kukamilika mwaka kesho kwa kujenga mitambo Minne ambayo itajengwa kwa awamu, kwa sasa mtambo mmoja uliopewa jina la Kinyerezi namba moja, ujenzi wake unaendelea na utakamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Ukikamilika utakuwa an uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawati 150 ambazo zitasaidia kupunguza gharama za kukodi Mashine za kuzalisha Umeme.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Injinia Fechesmi Mramba, amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kupunguza gharama za uzalishaji umeme ambapo kwa sasa inagharimu Senti 40 hadi 50 kwa Uniti Moja lakini baada ya kuanza kutumia Gesi gharama zitapungua hadi Senti Kumi kwa Uniti Moja.

No comments

Powered by Blogger.