Header Ads


Katika kuhitimisha kampeni za Ubunge jimbo la Kalenga CCM leo itafanya mkutano mkubwa wa aina yake kutokea katika jimbo la Kalenga kukiwa na viongozi mbali mbali kutoka ngazi ya Taifa na Jumuiya zake wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Kinana ambaye anaaminika kukirudisha Chama kwenye mstari kutokana na sera zake za uwazi na ukweli na kushirikiana vizuri na kila mwananchi wa Tanzania leo ataungana na mgombea Ubunge jimbo la Kalenga kupitia CCM Ndugu Godfrey Mgimwa kuhitimisha safari ndefu ya kampeni huko Kidamali.

PICHANI JUU: Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) ,Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) Mwigulu Nchemba (Kushoto) kwa pamoja wakiinua mikono juu pamoja na mgombea wa ubunge jimbo la Kalenga Ndugu Godfery Mgimwa .

Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa juu na wanachama na wapenzi wa CCM wakati akiingia kwenye viwanja vya mkutano Kalenga A. Moja ya sifa kubwa inayomuhakikishia ushindi Godfrey Mgimwa ni kutambua kuwa wana Kalenga ni ndugu zake ,wazazi wake, na marafiki zake na yupo tayari usiku na mchana kushiriki kuleta maendeleo ya jimbo hio.

No comments

Powered by Blogger.