Header Ads

Harry Kewell mbioni kustaafu


Aliyekuwa mchezaji wa Leeds United na Liverpool, Harry Kewell(Pichani) ametangaza kuwa `atatundika daruga' zake akiwa na umri wa miaka 35.

Mpaka sasa Raia huyo wa Australia amecheza mechi 250 akiwa katika ligi kuu ya soka ya Uingereza kuanzia mwaka 1995 mpaka 2008, akiwa na Leeds united na baadae Liverpool.

Kewell hivi sasa ni mchezaji wa klabu ya Melbourne Heart Fc ambayo pia imethibitisha kuwa nahodha wake huyo ataastaafu soka la kimataifa mwishoni mwa msimu huu wa ligi kuu soka Australia.

Mchezo wa mwisho kwa kewell utakuwa ni kati ya Melbourne Fc dhidi ya western Sydney Wonderes utakaopigwa AAMi Park katika mzunguko wa mwisho wa msimu wa ligi kuu soka Australia itakayopigwa April 12.

Akiwa Leeds Fc huko Uingereza, Kewell, alipewa tuzo ya (PFA Young Player) mchezaji bora kijana wa mwaka 1999 japokuwa baadae alihama na kutimkia Liverpool mwaka 2003.

No comments

Powered by Blogger.