Header Ads

DROO YA WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI YACHEZESHWA KIAINA YAKE JIJINI DAR.

Wiki iliyopita tiketi ya kwanza ya kwenda Brazili ilipata mwenyewe ambapo Deusdedit Kahwa ndiye aliyeibuka mshindi wa tiketi hiyo nkatika droo ya nne ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti. Katika droo hiyo pia walipatikana washindi wawili wa simu ya mkononi aina ya Samsung Gallaxy tab na washindi watano wa ving’amuzi. 

Wiki hii tena Kampuni ya Bia ya Serengeti imeendesha droo yake ya tano ya promosheni hiyo ambapo mshindi wa zawadi kubwa ya safari ya Brazili Bwana Kahwa ndiye aliyebonyeza kitufe cha kuzesha droo hiyo. 

Droo hiyo ilifanyika katika Kiwanda cha Bia cha Serengeti iliyoshuhudiwa na wana habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari, Afisa mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, PWC, push mobile media na mshindi wa droo ya nne ya promosheni hiyo. Promosheni hiyo bado ina wiki saba za kuendesha doo zake za kila wiki.


Washindi wa droo ya tano wa promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti ambao wamejishindia simu aina ya Samsung Gallaxy tab ni Daniel John kutoka Kirumba, Mwanza na Erick Mazigo kutoka Banana, Dar es Salaam.

Akizungumza kwa njia ya simu mshindi wa pili wa Samsung tab Erick Mazigo kutoka Banana, jijini Dar es Salaam, alielezea furaha yake kwa ushindi huo kwani hakutegemea kumiliki simu ya kisasa kama hiyo ingawa alishiri mara nyingi katika promosheni hiyo. 

Bwana Mazigo alisema, “ Naishukuru sana Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kujali wateja wake zawadi hii imenipa furaha sana kwani itanipa urahi wa kuperuzi vitu mbalimbali katika mtandao katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia”.

Naye Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo alieleza kuwa promosheni hiyo ambayo ilizinduliwa mwezi mmoja uliopita imeshagusa wanywaji wa bia ya Serengeti kwani wengi wameshajishindia bia za bure na fedha taslimu mpaka sasa zaidi ya wateja wetu 12,500 wameshajishindia fedha taslimu kupitia tarakimu walizozituma kwenda namba 15317. 

Aliongeza kuwa kila wiki washindi watano hujipatia ving’amuzi na kwa wiki hii alitangaza majina ya washindi wa ving’amuzi ambao ni Alex Lugiko  kutoka Kimara, Dar es Salaam, Alex Kishinde kutoka Nyakato, Mwanza, Astian Shirima kutoka Himo, Moshi, Hubart Lyatuu kutoka Mwanza na Victus Apengo kutoka Mbeya.

“Tunataka kuwakumbusha wateja wetu kuwa bado kuna zawadi kibao za kushindaniwa katika promosheni hii ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti ikiwemo ile kubwa zaidi ya Safari ya kwenda Brazili huku gharama zote zikilipiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti. Pia tuna zawadi zingine nyingi kama ving’amuzi, simu ya mkononi aina ya Samsung Gallaxt tab, bia za bure na pesa taslimu. Cha kufanya ni ndugu mteja kufungua bia yako ya Serengeti na uangalie chini ya kizibo jaribu leo unaweza kuwa mshindi wetu wa wiki ijayo. Tunapenda kuwashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono siku zote.” Alisisitiza Rugambo.


PICHANI JUU: Mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazili Deusdedit Kahwa akibonyeza kitufe kuchezesha droo ya tano ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti.
 Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tano ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti ilyofanyika jana katika Kiwanda cha Bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazili aliyepatikana wiki  iliyopita, Deusdedit Kahwa akielezea furaha yake kwa wana habari katika droo ya tano ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti iliyofanyika jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo.

No comments

Powered by Blogger.