Header Ads

Cheka kurejea toka `chimbo' Ijumaa hiiBondia wa ngumi za kulipwa Francis Cheka(Pichani) anatarajiwa kurejea nchini ijumaa Machi 28 akitokea Nairobi ulipokuwa kambi tayari kwa pambano lake dhidi ya Valery Brudov litakalopigwa April 5 mwaka huu katika ukumbi wa PTA Dar es salaam. 

Mratibu wa pambano hilo Mussa Kova amesema maandalizi ya pambano hilo yanaendelea vizuri pia kwa upande wa Cheka ataendelea kujiweka fiti kabla ya kumkabili bondia huyo kutoka nchini Urusi.

Cheka baada ya kukaa kambini Nairobi Nchini Kenya kwa siku 20 atarejea nchni na kufanya mazoezi katika kambi yake ya mjini Morogoro kabla ya kutua jijini Dar es salaam, kumkabili mpinzani wake.

No comments

Powered by Blogger.