Header Ads

Adhabu ya `Messi' kufikiriwa upya Uongozi wa klabu ya soka Simba umepanga kushusha adhabu nzito kwa mshambuliaji timu hiyo Ramadhani Singano `Messi' (Pichani) kwa kitendo cha utovu wa nidhamu. 

Messi alifanya utovu wa nidhamu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dae es salaam baada ya kumalizika kwa mchezo wao na Coasstal Union na kushindwa kuzuia hasira zake kwa kuamua kuvunja kioo cha uwanja wa Taifa.

Kitendo hicho kimetafsiriwa kama ni utovu wa nidhamu kwa uongozi wa Simba ambao ulitarajiwa kukutana kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ikiwemo sakata hilo.

Afisa habari wa klabu hiyo Asha Muhaji amesema bado hawajapata thamani ya kioo hicho kwa kuwa Mameneja wa uwanja wa Taifa hawajawasilisha Kwenye Shirikisho la soka Tanzania TFF na watakapo pata watalipa ila  Messi lazima apewe adhabu ya kukatwa mshahara.

No comments

Powered by Blogger.