Header Ads

15 wathibitishwa kupoteza maisha Bangui

Kiongozi Mmoja wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ametangaza kuwa, zaidi ya watu 15 wameuawa katika vitendo vya Ukatili vinavyoendelea kufanywa na makundi yenye Silaha Mjini Bangui nchini humo.

Kwa mujibu wa Afisa huyo, wanaharakati wa Shirika hilo wamekusanya Miili ya watu 15 kutoka katika eneo kulipotokea mapigano hayo.
 

Amesema mapigano hayo yametokea katika eneo la kibiashara la PK-Five Mjini Bangui.
 

 Kwa wiki kadhaa sasa Waislamu wamekuwa wakizingirwa na waasi wa Anti-Balaka katika eneo hilo.

No comments

Powered by Blogger.