Header Ads

BIA YA SERENGETI YAENDESHA DROO YAKE YA KWANZA YA KAMPENI ILIYOZINDULIWA HIVI KARIBUNI ‘WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI’!

Februari 12, 2014: Mawindo ya safari ya Brazili inayolipiwa gharama zote sasa ni juu ya wateja wa bia ya Serengeti ambao wamepata wiki iliyojaa zawadi kemkem kutoka bia za bure, pesa taslim na ving’amuzi vya kutosha. Asubui ya leo Kampuni ya Bia ya Serengeti imeendesha droo yake ya kwanza katika Kiwanda cha Bia cha Serengeti.

Droo iliyochezeshwa kiwandani hapo mapema leo, ilishuhudiwa na wana habari, maafisa waandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, PWC, na Push Mobile. Promosheni hii ya kurudisha fadhila kwa wateja itaendeshwa kwa wiki 11 zijazo.

Katika droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti wamepatikana washindi wawili wa (ipad) Mwl. John Yesaya(49) kutoka mkoani Kilimanjaro na Salehe Mohamed(25) kutoka jijini Dar es Salaam

Akizungumza kupitia simu ya kiganja mshindi wa IPAD Salehe Mohamed(25) kutoka jijini Dar es Salaam, alishikwa na butwaa na kujiona mwenye bahati mara baada ya kutamkiwa kuwa ni moja ya mshindi wa IPAD kupitia kampeni hii. Washindi hao hawakutegemea kuwa miongoni wa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni hiyo. Mshindi wa pili wa alielezea furaha yake na kuonekana kutoamini alichosikia. 


Washindi wote wawili waliishukuru Kampuni Kampuni yaBia ya Serengeti kwa kuwajali wateja wake siku zote na kuwatimizia mahitaji yao kwa kufanya vitu vya kustaajabisha kila kukicha alisema. Bwana Salehe alisema “kwakweli siamini, inanipa furaha na kujivunia kuwa mteja wa bia Serengeti. Kwa mimi kuwa mwenye bahati ya kupata (IPAD) ‘Samsung tablet’ inanipa ari kubwa hasa katika ulimwengu wa sasa wa dijitali.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Bwana Allan Chonjo alieleza kuwa promosheni iliyofunguliwa kwa wateja wote nchi nzima ambao wameshaanzankunufaika na kampenI hii. 


Zaidi ya wateja 172 wamejishindia fedha taslimu za kitanzania 5000, na wateja 130 wameshajishindia 10,000 ndani ya wiki hii ya kwanza ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti. Wote hao wamepata zawadi zao kupitaia simu ya kiganjani kwa kutuma maneno na tarakimu zilizopo chini yz kizibo kwenda namba 15317. 

Aliendelea kuelezea kuwa wateja wengi wameweza kufaidika zaidi kwani tangu uzinduzi wameweza kupata washindi wanne (4) waliojishindia ving’amuzi Robert M. Kitali kutoka Kilimanjaro, Deus P. Mwikitalu kutoka Buhongwa jijini Mwanza, Ali Hemed kutoka Mbezi jijini Dar es Salaam na Friimin R. Massawe
kutoka Kilimanjaro.

Tunataka kuwakumbusha wateja wetu kuwa bado tuna zawadi za kutosha za kushindaniwa katika promosheni hii kubwa zaidi ni ile ya safari ya Brazili itakayolipiwa gharama zote. Pia tunatoa ving’amuzi na IPAD kwa wateja wetu chakufanya ni wewe kufungua bia yako ya Serengeti kokote nchini na fuatilia maelezo ya promosheni na uweza kuwa mshindi wetu wa wiki inayokuja. Pia unaweza kufuatilia kupitia ukurasa wetu wa facebook www.facebook.com/serengetipremiumlager. 

Tumeanza vizuri hivyo hatuna budi kuwashukuru wateja wetu.“aliongeza Chonjo”
 

MAELEZO YA PROMOSHENI
Nunua chupa ya bia ya Serengeti, angalia chini ya kizibo. Ukipata picha ya bia ina maana unapata bia ya bure na unaichukua papo hapo. Ukipata tarakimu 6 za kipekee, tuma ujumbe mfupi wa tarakimu hizo kwenda nambari 15317 na utapata ujumbe papo hapo wenye majibu yafuatayo: kwamba umeshinda, umekuwa mshindi wa fedha taslimu kati ya shilingi 5000 na shilingi 10,000 ambayo mteja atatumiwa kupitia M-Pesa au atapata ujumbe mfupi kushukuru kwa kushiriki na kutaka kuendelea kushiriki. Hata hivyo kwa kushiriki tu, utaweza kuingia kwenye droo ambayo unaweza kujishindia safari ya brazil,
king’amuzi cha Azam na Ipad.
 

Gharama za kutuma ujumbe mfupi huu ni sawa na gharama ya kutuma ujumbe wa kawaida na unaweza kushiriki kupitia mtandao wowote. Safari ya Brazil itakuwa kati ya mwezi wa sita na saba mwaka huu.

Kwa maelezo zaidi fuatilia ukurasa wa kijamii wa facebook wa bia ya Serengeti.

PICHANI JUU: Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia  Serengeti Allan Chonjo akiongea kwa njia ya sinu na moja wa washindi wa droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti iliyochezeshwa mapema leo jijini Dar es Salaam kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo.  Ambapo washindi wawili wamejishindia 'Samsung tablets' ambao ni  Mwl. John Yesaya(49) kutoka mkoani Kilimanjaro na  Salehe Mohamed(25) kutoka jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo(kulia)akizungumza na wana habari(hawapo pichani)katika droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti, jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.