Header Ads

AIRTEL WAIPIGA JEKI MASHINDANO YA MPINGA CUP DAR 2013

 Kamanda msaidizi wa kikosi cha usalama barabarani, ACP Jehansen Kahatano (katikati) akipokea mipira itakayotumika kwenye mashindano ya Mpinga Cup. Anayekabidhi kushoto Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando pamoja na Raisi wa Be forward Tanzania Hironori Yamakawa. Katika makabidhiano hayo Airtel pia ilikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano kudhamini mashindano hayo ya Mpinga Cup. Anaeshudia ni Mkuu wa usalama barabarani kanda ya Dar es salaam ACP Amiri Konja (wakwanza kulia)
 Kamanda msaidizi wa kikosi cha usalama barabarani, ACP Jehansen Kahatano akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando iliyotolewa leo kwa dhumuni la kudhamini mashindano ya mpira wa miguu kwa waendesha pikipiki maarufu kama Mpinga cup. Anayeshuhudia katikati ni Raisi wa Be forward Tanzania Bw. Hironori Yamakawa na Mkuu wa usalama barabarani kanda ya Dar es salaam ACP Amiri Konja (wakwanza kulia).
======= ====== ======

Dar es salaam Novemba 1, 2013 

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa mara nyingine imeendelea kudhamini mashindano ya mpira wa miguu ya kila mwaka ya Mpinga cup Yenye lengo la kusaidia kutoa elimu kwa waendesha pikipiki ili kukabiliana na matukio ya ajali za barabarani.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi ya ya shilingi milioni 5 kwaajili ya kuendesha mashindano hayo Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema kampuni yake bado inaendelea na harakati za kuhakikisha inasaidiana na jeshi la usalama barabarani na wadau wengine wote ili kuhakikisha inapunguza idadi ya ajali barabarani kupitia njia yoyote ikiwemo michezo kama hii ya MPINGA CUP.

Airtel tumeamua kuyapiga tafu mashindano haya ya Mpinga cup kwa kuwa lengo lake ni kutimiza dhamira ya kijamii ya kupunguza na kutokomeza ajali barabarani , fedha hizi zitatumika kuendesha mashindano haya ya waendesha boda boda wa jijini Dar es salaam ambapo pia kupitia nafasi hii ya kukutana katika michezo tutaweza kutoa elimu ya uelewa wa usalama barabarani kwa lengo la kuwaokoa ndugu zetu na jamaa katika ajali zinazoepukika” alisema Mmbando.
 
Mbali na Airtel kampuni ya Be forward nayo imejitokeza kudhamini mashindano hayo kwa kutoa mipira 50 ili kuwezesha mshindano hayo yanayoshirikisha madereva wa piki piki maarufu kama bodaboda.

Akipokea msaada huo, Kamanda Msaidizi kikozi Usalama Barabara .Jehansen Kahatano aliwashukuru Airtel na Be forward kwa udhamini wao na kubainisha kuwa, mashindano ya mwaka huu yatakuwa na msisismko mkubwa kulinganisha na mwaka jana kwa kuwa ytayari yamepata mashabiki wengi na kuteka hisia za kiushindani kwa washiriki wa wilaya zote.

ninawashukuru sana Airtel Tanzania na kampuni ya Be forward kwa kutuunga mkono katika harakati zetu za kusambaza uelewa kwa watumia bara bara wote kupitia mashindano haya ya Mpinga Cup yanayoshirikisha waendesha bodaboda wa jijini dar es salaam, tunajua kuwa mashindano yamekuwa na yatakuwa na mvuto sana mwaka huu kwa kuwa tayari washiriki wote wamejipanga toka walipomaliza mashindano ya mwaka jana, sasa naomba tu niwakumbushe kuwa isiwe ni kushindania kwenye mpira tu bali pia tujiweke tayari kupokea elimu ya usalama barabarani ili tutimize pia lengo letu la kupunguza ajali barabarani” alisisitiza ACP Kahatano.

Mbali Airtel Kudhamini Mpinga Cup 2013 pia tunatumia vyombo vya habari ambavyo ni wadau wetu kuhakikisha wananchi au wadau wasomaji na watazamaji wa vyombo hivi wanapata habari za elimu hii ya usalama barabarani ili kuhakikisha tunasaidia jamii kupunguza athari zinazotokana na kukatishwa maisha kwa ghafla na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

No comments

Powered by Blogger.