Header Ads

ZAIDI YA WATU 380 WAKAMATWA KUTOKA NA VURUGU NCHINI RUSSIA

Zaidi ya watu 380 wamekamatwa jana nchini Russia baada ya vurugu kubwa iliyosababishwa na mhamiaji mmoja kumchoma kisu raia wa Russia jumatano iliyopita. 

Tukio hilo lilitokea eneo la kusini mwa mji mkuu wa Russia, Moscow. 

Vyombo vya habari nchini humo vinasema, waandamanaji wapatao 400 walivamia soko la mbogamboga kwenye jengo la maduka ambako wahamiaji wengi wameajiriwa kumsaka mtuhumiwa wa tukio hilo. Habari zinasema, mtuhumiwa wa tukio hilo mwenye asili ya Asia ya kati alikimbia mara baada ya kumchoma kwa kisu Yegor Shcherbakov, raia wa Russia. 

Meya wa mji wa Moscow Sergey Sobyanin ameamuru kituo cha dharura kianzishwe kushughulikia suala hilo. Polisi wanasema wamedhibiti vurugu hizo na askari 5 wamejeruhiwa katika mapigano kati ya waandamanaji na polisi. 

Kufuatia tukio hilo, raia wa kigeni wameaswa kutotembea hovyo mjini Moscow.

No comments

Powered by Blogger.