Header Ads

WATOTO 5855 HAWAJUI KUSOMA WALA KUANDIKA MKOANI KATAVI


  UWEZO WASHIRIKIWASHIRIKI WA KWENYE SEMINA WAKIFUATILIA NAMNA MAFUNZO  YA UWEZO TWAWEZA.
…………………………………………………………………………

Na Kibada Kibada –Mpanda Katavi

Jumla ya watoto 5855 hawajui kusoma wala kuandika katika mkoa wa Katavi kufuatia utafiti uliofanyika kwa baadhi ya maeneo mkoani Katavi hivyo kuonesha kuwa wapo watoto wengi wasiojua kusoama na kuandika katika mkoa huo.

Hayo yamebainishwa  katika warsha ya wahojaji wa kutoka Jitihada binafisi za wananchi UWEZO TWAWEZA inayoendesha nchi nzima na Afrika Mashariki kwa ajili ya kuwabaini watoto wasiojua kusoma na kuandika katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa Mratibu wa UWEZO  Mkoa wa Katavi Godfrey Mogella alieleza kuwa shughuli za uwzo zinafanyika  Afrika Mashariki na tangu kuanza katika mkoa wetu kwa sasa ni miaka mitatu zoezi hili lilianza mwaka 2010 kuweza kuwatambua  watoto.

kifafanua zaid alieleza kuwa hawa wahojaji waliopo hapa watapatatiwa amafunzo kwa muda wasiku mbili kisha wataenda kufanya zoezi hili katika maeneo mbalimbali yaliyobainishwa kwa ajili ya kufanyia utafiti huo.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Mhandisi Emanuel Kalobelo akifungua Warsha hiyo ametoa Changamoto kwa wahojaji hao kufanya kazi kwa uamini wa hali ya juu kwa kuwa matokeo ya tafiti hizo yatatumika kuleta mafaniki katika kuboresha elimu hapa nchini.

Akasisitiza kutumia lugha ya maadili itakayosaidia kuweza kuelewana na wale wanaohojiwa kwa kutoa maneno na lugha nyepesi ambayo kila mmoja ataweza kuielewa bila matatizo isilete migongano katika jamii aliwasihi wajishushe ili kuendana na wale wananchi wa kijiji kuweza kuendana nao.

“Iwapo mtatumia lugha za ajabu ni heri ujiondoe mapema kuliko kujiingiza na kufanya kitu ambacho huwezi kutekeleza kutoka moyoni na kufanya kazi kwa uamini na kwa uzalendo wa kuipenda nchi”alisema Mhandisi Kalobelo.

Alisema seikali itajitahidi kutumia matokeo ya tafiti hizo kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na mstakabali wa nchi hii kwa kizazi kilichopo na kijacho.

No comments

Powered by Blogger.