Header Ads

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA POLISI MBEYA


DSC00260

WILAYA YA  CHUNYA – MAUAJI.

MNAMO TAREHE 07.10.2013 MAJIRA YA  SAA 08:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MTANILA WILAYA YA  CHUNYA  MKOA WA MBEYA. THOBIAS S/O KILIAN @ ZAMBI, MIAKA 68, MBUNGU,  MKULIMA,  MKAZI WA KIJIJI CHA MTANILA ALIKUTWA AMEUAWA NYUMBANI KWAKE KWA KUKATWA PANGA KICHWANI, SHINGONI NA MIKONONI  NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

 MBINU NI KUMVAMIA  MAREHEMU AKIWA AMELALA CHUMBANI KWAKE PEKE YAKE  NA KUMUUA. CHANZO NI IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI MAREHEMU ALIKUWA ANATUHUMIWA KUWA NI MCHAWI NA PIA YEYE MWENYEWE ALIKUWA ANATAMBA KUWA ANA UWEZO WA KICHAWI NA AMESHINDIKANA HAPO KIJIJINI. 

MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI WA SERIKALI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA KUSADIKI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII.


WILAYA YA  MOMBA –   AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 07.10.2013 MAJIRA YA  SAA 15:00HRS HUKO KATIKA KJIJI CHA CHAPWA BARABARA YA  MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA  MOMBA MKOA WA MBEYA. GARI T.952 CES AINA YA  TOYOTA NOAH LIKIENDESHWA NA DEREVA UTHENT S/O NDAMBO, MIAKA 54, MHEHE, MKAZI WA TUNDUMA LILIMGONGA MPANDA BAISKELI ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA  KIUME, MWENYE UMRI KATI YA  MIAKA 20-25 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI

 MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA  ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.WILAYA YA  MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.

MNAMO TAREHE 07.10.2013 MAJIRA YA  SAA 19:30HRS HUKO ENEO LA KABWE  JIJI NA MKOA WA MBEYA. 
 
ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JACOB S/O SWALO, MIAKA 26, KYUSA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA SINDE AKIWA NA NOTI BANDIA SABA [07] @ TSHS 5,000/= ZENYE NAMBA BD-0380040 SAWA NA TSHS 35,000/=   NA NOTI 2  TSHS 10,000/= ZENYE NAMBA CX- 4841211 SAWA NA TSHS 20,000/= . 
 
 TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA  PESA HASA NOTI ILI KUJIEPUSHA NA MATAPELI /WALAGHAI WANAOTAKA KUJIPATIA KIPATO NA UTAJIRI KWA NJIA ZISIZO HALALI.WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU.

MNAMO TAREHE 07.10.2013 MAJIRA YA SAA 16:40HRS HUKO META JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA AMOS S/O GIDION, MIAKA 29,  KYUSA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA MABATINI  AKIWA NA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AMBAZO NI POMBE KALI AINA YA  DOUBLE PUNCH KATONI 4, MASTER KATONI 1 NA BOSS KATONI 1. 

MBINU NI KUSAFIRISHA POMBE HIZO KWA KIFICHO AKIWA KATIKA GARI LA KUBEBA ABIRIA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAMLAKA YA  MAPATO [TRA] NA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA [TFDA]                                                                                                                                                                                                                                                            KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

 by:
 [DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments

Powered by Blogger.