Header Ads

STEVE NYERERE AITAMBULISHA FILAMU YAKE MPYA LEO JIJINI DAR,KUSAMBAZWA NA KAMPUNI YA PROIN PROMOTIONS


Pichani kati ni  mmoja wa wasanii  mahiri katika tasnia ya Uigizaji wa filamu Tanzania, Steven Megele almaarufu Steve Nyerere akifafanua kuhusiania na ujio wa filamu yake mpya iitwayo Long Time,mbele ya baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani), alipokuwa akizungumza nao kwenye ofisi ya Kampuni ya Proin Promotions  zilizopo Mtaa wa Ursino Jijini Dar.Filamu hiyo pia itasambazwa na kuuzwa na  Kampuni ya Proin Promotions Limited kupitia Mawakala wao Nchini Nzima kuanzia leo
 Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano na Msanii wa Filamu Tanzania Steve Nyerere akiwa pamoja na Meneja masoko Wa Proin Promotions Bw Evans Stephen wakati wakiitambulisha filamu hiyo mpya kutoka Proin Promotions iitwayo Long Time
Pichani kulia ni Meneja Masoko wa kampuni ya Proin Promotions Bw Evans Stephen akiongelea juu ya ujio wa filamu ya Long Time iliyoigizwa na Wasanii mahiri Steve Nyerere na Johari.Filamu hiyo imetengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited na itasambazwa na kuuzwa na Mawakala Wa Proin Promotions Limited Nchini Nzima na itaanza kupatika leo katika Sehemu Mbalimbali za Tanzania.
 
=======  ======  =========
Kampuni ya utengenezaji,uuzaji na usambazi wa filamu za kitanzania Kutoka nchini Tanzania ya Proin Promotions leo imetambulisha rasmi filamu yake mpya iitwayo Long Time ambayo itapatikana kuanzia leo sokoni kwa gharama ya Shilingi Elfu tano tu za kitanzania

Filamu ya Long Time ni filamu ambayo imetengenezwa na kampuni mahiri ya Proin Promotions limited na kuigizwa na wasanii wakongwe na nguli wakiwemo Steve Nyerere, Blandina Chagula na wengine wengi.

Proin Promotions limited imejikita katika kubadilisha soko la filamu Tanzania na kuleta mapinduzi ya kweli katika tasnia ya filamu nchini,Na  takribani nakala laki moja za Filamu ya Long Time zishaingia soko leo na kuuzwa. Long Time ni filamu ambayo inafundisha na kuburudisha na pia inayoelezea Uhalisia wa maisha ya Mtanzania.

Jinsi ya Kupata nakala yako ya Long Time unaweza kutembelea maduka yanayouzwa filamu za kitanzania na Kwa Mawakala Wote wa Proin Promotions Wanaopatikana Nchi Nzima Vilevile unaweza kuagiza oda yako ya filamu za Proin Promotions Limited kupitia tovuti yao ya www.proinpromotions.com na katika ukurasa wao wa facebook kwa kulike ukurasa huo bofya kiunganishi  https://www.facebook.com/proinpromotions.

No comments

Powered by Blogger.