Header Ads

SEKTA BINAFSI YAASWA KUJA NA HUDUMA ZINAZOKIDHI WATU WA KIPATO CHA CHINI

DSC_0167
SERIKALI imeitaka sekta binafsi katika usafiri na usafirishaji kuja na bidhaa huduma ambazo zinamlenga mtu wa kipato cha chini na zinakidhi mahitaji ya wananchi katika juhudi za kuboresha maisha ya watanzania kupitia sekta ya uchukuzi nchini. Moblog linaripoti.
Akizungumza na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi rasmi wa Bima ya Safari Njema jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Uchukuzi na Usalama toka Wizara ya Uchukuzi, Bi Tumpe Mwaijande ambaye alikuwa anasoma hotuba ya Waziri Dk Harrison Mwakyembe amesema sekta ya uchukuzi ni nguzo muhimu katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
“tunawashukuru African life Assurance na Ndege Insurance Brokers kwa kuja na huduma hii mpya kwa wananchi lenye lengo la kupunguza machungu na makali ya maisha endapo itatokea ajali au ulemavu wakati wa safari, huu ni mfano wa pekee katika ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi katika kumletea mwananchi maendeleo,” amesema.
PICHANI JUU: 
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uchukuzi na Usalama kutoka Wizara ya Uchukuzi, Bi. Tumpe Mwaijande akizungumza na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi rasmi wa bidhaa mpya kabisa ya bima nchini Tanzania “Safari Njema” mahsusi kwa wasafiri.
DSC_0131
Mkurugenzi Mtendaji wa Ndege Insurance Brokers, Dk Sebastian Ndege akitoa hotuba yake na kuelezea jinsi huduma hii ya safari njema bima itakavyofanya kazi kwa wasafiri hapa nchini.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi inaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha maisha ya watanzania yanalindwa wakati wapo safarini kwa kuwaletea bima ya safari njema yenye bei na viwango nafuu ili kumwezesha mtu wa kipato cha chini kumudu gharama hizo.
Mwaijande amesema taifa kila siku kupoteza nguvu kazi kwa sababu ya ajali za mara kwa mara ambazo wahanga wa ajali mara nyingi kuachwa bila fidia lakini baada ya uzinduzi huu wa bima ya safari njema kwa wasafiri ni mkombozi wa kweli kwa watanzania.
“Huduma hii ya Safari njema bima kwa wasafiri nchini ni mkombozi wa kweli kwa wahanga wa ajali endapo itatokea ulemavu au kifo kwa wasafiri basi wanaweza kufidiwa au kutibiwa,”alisisitiza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Ndege Insurance Brokers, Dk Sebastian Ndege amesema vifo na ulemavu vitokanavyo na ajali ni moja kati ya adui mkubwa wa maendeleo ya mtanzania.
DSC_0144
Afisa Mtendaji Mkuu wa African Life Assurance, Ndg Julius Magabe akizungumza na wageni waalikwa wakati uzinduzi rasmi wa bidhaa mpya ya safari njema bima kwa watanzania jijini Dar es Salaam katika stendi ya mabasi Ubungo.

Amesema kuwa endapo itatokea kifo, mrithi alietajwa atalipwa Tsh 10m na ulemavu wa kudumu mbima atalipwa kiasi cha Tsh 10m kwa kupitia njia rahisi ya (Mobile Money) kama vile Mpesa, Tigopesa, Airtel Money na Zpesa.
“Takwimu zinazonyesha, kati ya Januari na Disemba 2012, zilitokea ajali 23,000 ambapo watu wapatao 5,320 walipoteza maisha na ukichukua wastani wa utegemezi wa watu wanne kila marehemu mmoja, ni sawa na wahanga elfu ishirini kwa kila mwaka
‘Pale unapokua safarini, unachotakiwa kufanya ni kupiga kwenda number Nyota -150-nyota-23-alama ya reli na utapata maelezo ya BIMA hii ni jinsi ya kujiunga utahitajika kujaza taarifa muhimu kama jina lako, tarehe ua kuzaliwa, jina la mrithi na namba yake ya simu,” amesema Ndege
Dk Ndege amesema Ndege insurance kwa kushirikiana na African Life Assurance imeona umuhimu wa kubuni bidhaa inayomjali mtanzania wa kipato cha chini kuweza kumudu Bima za ajali safarini kwa bie nafuu.
Dk Ndege aliendelea kusema kuwa kupitia bidhaa yao mpya wamejiandaaa kutoa elimu kwa umma ju ya umuhimu wa BIMA ya maisha kwa watanzania na pia kuhakikisha inapatikana kwa urahisi na wananchi.
DSC_0156
Mwenyekiti wa Bodi ya African Life Assurance na Waziri wa Zamani Ibrahim Kaduma akizungumza na wageni waalikwa na kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa shughuli hiyo.
Akiielezea bima ya safari njema, Bw Julius Magabe, Afisa Mtendaji Mkuu wa African Life Assurance, amesema uanzishwaji wa bima ya safari njema unaendana na dhima ya African life ya kuboresha maisha ya watanzania kupitia upatikanaji wa bima za maisha.
“Ni matazamio yangu kuwa, kiwango kidogo cha ukataji wa bima ya safari njema cha shilling 5,000 kitawawezesha watanzania wengi kuipata huduma hii muhimu kwa wasafiri wa mbali na hata wale waendao kwenye shughuli za kila siku,” amesema Magabe
Ndege Insurance Brokers kwa kushirikiana na African life Assurance kampuni ya bima ya maisha wamezindua rasmi huduma ya bima ya maisha kwa wasafiri wa mabasi, magari, daladala, meli na ndege. Bima hii ya maisha yenye kutoa mafao kwa watakaokata bima wakati wakisafiri.
Safari Njema ndio jina maalumu bima hii ya maisha ya wasafiri, sasa kila msafiri anaweza kukata bima ya maisha safari njema inayotoa kinga ya siku 7 uwapo safarini.
DSC_0148
Picha juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa Safari Njema huduma mpya ya bima kwa wasafiri nchini.
DSC_0146
DSC_0154
DSC_0168
Mgeni rasmi Bi Tumpe Mwaijande akikata utepe kuashiria huduma mpya ya Bima ya wasafiri "Safari njema" imezinduliwa rasmi jijini Dar leo, Kulia ni Dk. Sebastian Ndege na Julius Magabe.
DSC_0169
Mgeni rasmi Bi Tumpe Mwaijande akifungua kitambaa cha utepe wakati wa uzinduzi.
DSC_0171
Sasa imezinduliwa rasmi Watanzania kazi kwenu jali maisha yako na familia yako pindi unaposafiri itakugharimu Tshs 5000/=.
DSC_0172
Dr. Sebastian Ndege akipeana mkono na Mgeni rasmi Bi.Mwaijande.
DSC_0178
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Ryan Bert and Compay Limited na Swordfish Security Consultants Haki Ngowi (mwenye miwani mweusi) naye alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo.
DSC_0180
Mgeni rasmi Bi. Mwaijande akiondoka eneo la tukio baada ya uzinduzi.
DSC_0186
Afisa Mtendaji Mkuu wa African Life Assurance Ndg Julius Magabe na Mkurugenzi Mtendaji wa Ndege Insurance Brokers, Dk Sebastian Ndege wakipeana ya kheri baada uzinduzi wa Huduma yao mpya ya Bima ya Safari njema katika soko la Tanzania.
DSC_0202
Dk Sebastian Ndege akibonyeza mashine ya kodi maalumu EFD toka TRA wakati wa uzinduzi rasmi wa safari njema bima ambayo ni bidhaa mpya katika soko la Tanzania.
DSC_0205
Wakili Justin Ndege (kulia) akiwa na wadau wengine wakati wa uzinduzi wa bima ya Safari njema.

No comments

Powered by Blogger.