Header Ads

RC KATAVI AWATAKA WATUMISHI WA SEKTA YA BARABARA KUWAJIBIKA IPASAVYO, KUWACHUKULIA HATUA KALI WAKIZEMBEA


MENEJA WA BARABARA 
Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoani Katavi,  Mhandisi Isack Kamwela akitoa taarifa ya hali ya mtandando wa barabara na shughuli za utekelezaji wa ujenzi wa barabara katika mkoa jinsi inavyoendelea kwenye kikao cha tatu cha bodi ya barabara leo.
KAMATI YA ULINZI MKOA 
Baadhi ya wajumbe wa waliohudhuria kikao cha bodi ya bararabara Mkoa wa Katavi wakifuatilia mjadala wa Kikao cha barabara kwa mstakabali wa maendeleo ya Mkoa wa Katavi.
(Picha na Kibada Wakibada)
………………………………………………………………

Na Kibada Kibada –Mpanda Katavi.  
Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Dkt Rajabu Rutengwe ametoa Changamoto kwa watumishi wa Sekta ya Barabara kuwajibika na hatosita kuwachukulia hatua iwapo watashindwa kuwajibika kwa  watumishi hao.

Changamoto hiyo ameitoa wakati akifungua wa Kikao cha Pili cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi kilichofanyika kwenye  ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ulioko Idara ya Maji Mjini Mpanda Mkoa wa Katavi leo.

Dkt Rutengwe amesema hatoona aibu kumchukulia hatua mtumishi yeyote atakayeshindwa kusimamia kazi kwa kiwango kinachotakiwa hadi kufika utekelezaji wa kazi inayokidhi viwango.
Alitoa changamoto hiyo kufuatia kupokea taarifa za utekelezaji wa kazi za ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali ikiwemo barabara ya kutoka sumbawanga  Mpanda hasa eneo la mbungani ambalo linajengwa kwa kiwango cha vumbi .

Ameseka kuwa kazi bado hazijakamilika na mkandarasi anayejenga eneo hilo amekuwa akifanya kazi kwa taratibu sana hali inayofanya kazi isikamilike kwa wakati ya ukarabati
Kufuatia utendaji kazi huo ambao huuridhishi ameagiza kuwa mkandarasi anayejenga barabara hiyo ya Vumbi asipewe Certificate ya kulipwa fedha hadi mamlaka husika akakague kazi hiyo imefikia hatua gain ya kazi.

Katika Hatua nyingine kwa nyakati tofauti Wanyeviti wa Halmashauri ya Wilaya Mlele Wilbrod Mayala ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Ahamed Mohamed na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Enock Gwambasa na Katibu wa CCM Mkoa Alphonce Kinamhala walilalamikia Wakala wa Barabara kwa kuweka alama ya kwenye nyumba zilizoko kandokando ya barabara nyumba ambazo zinatakiwa kubomolewa na kupisha ujenzi kuwa hawajalipwa fidia yao.

Waliomba kulipwa kwa wananchi hao ili kuondoa kero wanayoipata wananch nap engine kuipunguzia serikali kulaumiwa kutokana na kitendo hicho cha kutokulipwa wananchi wao kwa kufanya hivyo wananchi wanaichukia serikali yao bure ni vyema utaratibu ukaangaliwa upya walipwe fedha zao wananchi za Fidia.

Kwa Meneja wa Barabara Mkoa wa Katavi Isaack Kamwelwe alitolea ufafanuzi juu ya watu waliowekewa alama za kijani kuwa wote watalipwa isipokuwa taratibu za kiserikali hazijakamilika na hilo ni tatizo karibu la nchi nchi lakini hakuna mtu hata mmoja ambaye hatalipwa fidia yake tatizo hilo linashughulikiwa.

No comments

Powered by Blogger.