Header Ads

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. PEREIRA SILIMA AFUNGUA KIKAO CHA BAJETI YA SHIRIKA LA MAGEREZA LEO MKOANI MOROGORO

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(Mb) mapema leo Oktoba 21, 2013 alipowasili katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro tayari kwa ufunguzi rasmi wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. Wa pili kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga. 2 
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kuhusu Maendeleo ya Shirika la Magereza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima( hayupo pichani) kufungua rasmi Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 kinachofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro. 3 
Naibu Wazir wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(Mb) akisoma hotuba ya ufunguzi wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza ya Mwaka wa Fedha 2013/2014 kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 21, 2013 katika Ukumbi wa Edema, Mkoani Morogoro. 4 
Baadhi ya wajumbe wanaoshiriki Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa mwaka wa fedha 2013/2014 wakiwemo Wakuu wa Magereza Mikoa yenye miradi ya Shirika pamoja na Wasimamizi Wakuu wa Miradi  hiyo wakisikiliza  hotuba ya Mgeni katika ufunguzi wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza ambacho kimeanza leo   Oktoba 21, 2013 katika Ukumbi wa Edema, Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima( wa tatu kulia) akifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 leo Oktoba 21, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro( kushoto kwake) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja( Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza). 6 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima((wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Magereza yenye miradi ya Shirika mara baada ya kufungua  rasmi Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 leo Oktoba 21, 2013 katika Ukumbi wa Edema, Morogoro( wa tatu kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja( wa pili kushoto) ni Kamishna Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile. Wengine ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa( wa pili kulia) na Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga( wa kwanza kulia). Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.

No comments

Powered by Blogger.