Header Ads

DK RAJABU RUTENGWE AWATAKA WATUMISHI WA SEKTA MBALIMBALI MKOANI KATAVI KUWAJIBIKA KWA NAFASI ZAO


Dakta-Rajabu-Rutengwe 

Na Kibada Kibada –Mpanda Katavi.
  Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Dkt Rajabu Rutengwe ametoa Changamoto kwa  watumishi   wa Sekta  mbalimabali Mkoani humo kila mmoja kwa nafasi yake hususani  Sekta ya Barabara kuwajibika na hatosita kuwachukulia hatua iwapo watashindwa kuwajibika  katika nafasi zao walizokabidhiwa na serikali kwa ajili ya kusimamia majukumu yao ya kazi.  

Changamoto hiyo ameitoa wakati wa Kikao cha Pili cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Katavi kilichofanyika kwenye  ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ulioko Idara ya Maji Mjini Mpanda Mkoa wa Katavi alipokuwa akifungua na kuwaasa wajumbe wa kiao hicho pamja na waalikwa wa kikao hicho.

Dkt Rutengwe amesema hataona aibu kumchukulia hatua mtumishi yeyote atakayeshindwa kusimamia kazi kwa kiwango kinachotakiwa hadi kufika utekelezaji wa kazi inayokidhi viwango kwa mjibu wa taratibu kila mmoja kwa nafasi yake katika eneo lake..

Alitoa changamoto hiyo kufuatia kupokea taarifa za utekelezaji wa kazi za ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali ikwemo barabara ya kutoka sumbawanga  Mpanda hasa eneo la mbungani ambalo linajengwa kwa kiwango cha vumbi.

 Amesema katika barabara hiyo  kazi bado hazijakamilika na mkandarasi anayejenga eneo hilo amekuwa ikifanya kazi kwa taratibu sana.na kuchelewesha ukamilishaji wa kazi.
Kutokana na  utendaji huo    ambao huuridhishi ameagiza kuwa mkandarasi anayejenga barabara hiyo ya Vumbi asipewe Certificate ya kulipwa fedha hadi mamlaka husika zikakague kazi  imefikia hatua gani  ndipo apatiwe cheti cha kumwezesha kulipwa malipo yake ya  kazi.
 
Katika Hatua nyingine  kumejiokeza malalamiko kutoka kwa wajumbe wa kikao ambao ni  Wenyeviti wa Halmashauri zaa Wilaya ya Mlele  Wilbroad Mayala ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Ahamed Mohamed na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Enock Gwambasa , Katibu wa CCM Mkoa Alphonce Kinamhala  pamoja na Msaidizi wa Waziri Mkuu Jimbo la Charles Kanyanda kulalamikia Wakala wa Barabara kwa kuweka alama za kijani kwenye nyumba za wananchi zilizoko kandokando ya barabara  ambazo wanatakiwa wapishe ujenzi wa barabara ya lami lakini hawajui hatima yao na watalipwa lini, nyumba ambazo zinatakiwa kubomolewa na kupisha ujenzi wa barabara na wananchiwengine walishaanza kuzibomoa lakini bado hawajalipwa  hawajalipwa fidia yao na hawajui hatima yao.

Waliomba kulipwa kwa wananchi hao ili kuondoa kero wanayoipata wananch na pengine kuipunguzia serikali  mzigo wa kulaumiwa kutokana na kitendo hicho cha kutokulipa wananchi hao kwa kufanya hivyo wananchi wanaichukia serikali yao bure ,ni vyema utaratibu ukaangaliwa upya walipwe fedha zao wananchi za Fidia.

Kwa  upande wake Meneja wa Barabara Mkoa wa Katavi Isaack Kamwelwe alitoa ufafanuzi juu ya watu waliowekewa alama za kijani kuwa wote watalipwa isipokuwa taratibu za kiserikali hazijakamilika na hilo ni tatizo karibu la nchi nzima lakini hakuna mtu hata mmoja ambaye hatalipwa fidia yake wote watalipwa jambo la msingi wafanye uthamini wa mali yake ikiwemo nyumba na tatizo hilo linashughulikiwa.

No comments

Powered by Blogger.