Header Ads

CCM YAMTUMIA SALAMU ZA PONGEZI RAIS MPYA WA TFF JAMAL MALINZI

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza Rais Mstaafu wa Shirikisho la Mpira nchini (TFF) Leodger Tenga kwa uongozi wa kutilia mfano uliowezesha kuleta mapinduzi makubwa ya mifumo ya soka nchini.

Aidha CCM inamtumia salam za pongezi za dhati Rais Mpya wa TFF, Jamal Malinzi, na Uongozi wake wote mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliopatikana katika uchaguzi uliofanyika juzi, Oktoba 27, 2013 jijini Dar es Salaam.

Chama Cha Mapinduzi, kinaimani kubwa na Malinzi wa wenzake katika kuendeleza jitihada zilizoanzishwa na uongozi uliomaliza muda wake sanjari na kuibua mbinu mpya zitakazoboresha na kuleta mapinduzi makubwa ya soka nchini.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye anawaasa“Tunauomba uongozi mpya kujiepusha na jitihada za kujiendeleza binafsi na badala yake uwekeze katika soka na kuepusha migogoro isiyo na tija katika mchezo huo ambao kwa sasa ndio unaopendwa na Watanzania wengi”

“Daima imani huzaa imani, hivyo imani ya CCM kwako na kwa viongozi wenzako mliochaguliwa pamoja izae imani ya utumishi uliotukuka"  Ndugu Nape amehitimisha.


Chama Cha Mapinduzi kinatambua kuwa migogoro imekuwa kwa sehemu kubwa chanzo cha kukwamisha sana maendeleo ya soka hapa nchini na hivyo kuwanyima Watanzania raha ambayo huitarajia kutoka kwenye mchezo huo na hasa pale timu zao zinapopata ushindi.
Imetolewa na:-

Kitengo cha Mawasiliano na Umma
Chama Cha Mapinduzi
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu

Dar es Salaam

No comments

Powered by Blogger.