Header Ads

WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI YAKUTANA NA WANAHABARI NA KUELEZA MIKAKATI YAKE


IMG_5034 
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakitazama moja ya mabwawa yanayotumika  kufugia  samaki katika mradi unaoendeshwa na William  Bwemelo katika eneo la Pugu Kinyamwezi  kwa msaada wa Wataalamu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. IMG_4957 
Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Mohamed Bahari akiwaeleza waandishi wa habari  kuhusu mikakati ya  Serikali  katika kukabiliana na upungufu wa samaki nchini kwa kutoa msukumo  kwa wananchi kuanzisha miradi ya ufugaji wa samaki katika maeneo yao. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi Bahari Kuu Zahor El Kharousy. IMG_4974Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Uvuvi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Fatma Sobo akiwaeleza  waandishi wa habari juu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na Uvuvi haramu hapa nchini. IMG_5010 
Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Dr. Baraka Kuguru  akifafanua kwa waandishi wa habari  namna bora ya kukuza vifaranga vya samaki wakati walipotembelea mradi huo. IMG_4961 
Baadhi ya Waandishi wa habari wakisikiliza maelezo toka kwa Msemaji  wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Mohamed Bahari akiwaeleza  kuhusu mikakati ya  Serikali  katika kukabiliana na upungufu wa samaki nchini wakati  walipotembelea moja ya miradi ya ufugaji samaki katika eneo la Pugu Kinyamwezi jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.