Header Ads

WATUMIAJI WA TAKWIMU AMBAZO SI SAHIHI WAPEWA ONYO MAPEMA, SHERIA INAPIKWA JIKONI!!

IMG_4486IMG_4510 
Kamishna  wa Sensa ya  Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Hajjat Amina Mrisho akizungumza na waandishi wa habari leo  kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) kuhusu uzinduzi wa kitabu cha pili  cha idadi ya watu cha umri na jinsi, ambacho kitasaidia kupanga mikakati mbalimbali ya kimaendeleo.
Picha na Magreth Kinabo – Maelezo
………

Na Magreth Kinabo- Maelezo
KAMISHNA wa Sensa ya  Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Hajjat Amina Mrisho ametoa onyo kwa watu wanaotumia takwimu ambazo si sahihi  wanapotoa taarifa mbalimbali kuwa wawe makini kwa kuwa sheria  ya kuwabana iko mbioni.
 
Aidha  Hajjat Amina   amesema  kwamba kwa watendaji wa Serikali, na wanasiasa  watakaotoa takwimu za uongo katika taarifa mbalimbali  wajiandae kuong’ooka  katika nyadhifa zao.
 
Kauli hiyo imetolewa leo na Kamshina huyo wakati  akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) kuhusu uzinduzi wa kitabu cha pili  cha idadi ya watu cha umri na jinsi, ambacho kitasaidia kupanga mikakati mbalimbali ya kimaendeleo.
 
“Muswada wa Sheria ya   Takwimu wa mwaka 2013 imeshasomwa mara ya kwanza Bungeni ,unasubiriwa  kusomwa kwa mara ya pili katika Bunge lijalo. Hivyo  itakapokamilika  sisi tutapambana na watu wanaotoa takwimu ambazo si sahihi. Kwa watendaji wa Serikali watakaotumia takwimu ambazo si sahihi wakati wanapotoa taarifa mbalimbali mfano tatizo la njaa linawakabili watu kiwango  kipi  wajiandae kufukuzwa kazi,” alisema Hajjat Amina.
 
 Alisema suala linatakiwa pia kuzingatiwa watu wataotangaza au kuandika,wakiwemo waandishi wa habari  takwimu zilizotajwa na mtu bila ya kufanyiwa uchunguzi kupitia mtandao wa ofisi hiyo watachukuliwa hatua kulingana na sheria hiyo.
 
Hajjat Amina alifafanua kuwa takwimu hizo zitakuwa zitaboreshwa kwa kila mwaka, hivyo aliwataka watu kuzitumia ipasavyo  kulingana na taarifa za kila mwaka.
 
Akizungunzia kuhusu uzinduzi huo, alisema utafanyika Septemba 25, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo jijini Dares Salaam, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi  Sief  Ali Iddi .
 
Aidha Hajjat Amina aliongeza kuwa  ofisi hiyo itato vitabu 2 , kitabu cha tatu kuhusu takwimu za walemavu kifuata kitazinduliwa mwishoni mwa mwezi wa Okctoba na cha nne kitakachoonesha  takwimu za kila mkoa, utakuwa na chake.

No comments

Powered by Blogger.