Header Ads

PIGO ARSENAL, PODOLSKI ATAKIWA KUWA NJE MIEZI MITATU

BAADA ya kumsajili Mesut Ozil kwa dau la Pauni Milioni 42.5 katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa pazia jana, Arsenal imepata pigo kufuatia kuambiwa Lukas Podolski anatakiwa kuwa nje kwa miezi mitatu kwa sababu ya majeruhi.
 
Dawati la Madaktari la Arsenal tayari lilikubali kumkosa mshambuliaji huyo kwa wiki kati ya nane na 10, lakini madaktari wenzao wa timu ya taifa ya Ujerumani, walifanya uchunguzi wa kina na kusema Podolski ana muda mrefu wa kuwa nje.
 
Dk Hans-Muller Wohlfahrt, ambaye alishughulikia vipimo vya afya vya Ozil kwa niaba ya Arsenal kiungo huyo akiwa Ujerumani kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Austria Ijumaa, alituma taarifa hizo Gunners leo. 
 
Welcome aboard: New Arsenal team-mates Lukas Podolski (left) and Mesut Ozil (right) pose with a club shirt
Karibu kwetu: Podolski akiwa na mchezaji mwenzake mpya wa Arsenal, Mesut Ozil (kulia) na jezi ya klabu hiyo
Blow: Lukas Podolski has been ruled out of action for up to three months with a hamstring injury
Pigo: Podolski anatakiwa kuwa nje kwa miezi mitatu kutokana na maumivu ya nyama

Muller-Wohlfahrt alimfanyia vipimo Podolski mjini Munich na kugundua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amechanika nyama katika mguu wake wa kushoto na atakuwa nje hadi Desemba.
 
Podolski ameliambia gazeti la kila siku la Ujerumani, Bild: kwamba "Kwa bahati mbaya nitakuwa nje kwa muda mrefu kiasi cha miezi mitatu,". 
 
Record breaker: Mesut Ozil has arrived from Real Madrid in a colossal £42.5m deal
Munja rekodi: Mesut Ozil amewasili kutoka Real Madrid kwa dau la Pauni Milioni 42.5

Podolski alitolewa nje ya kikosi cha timu yake kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Fenerbahce wiki iliyopita. Na licha ya kusajiliwa kwa Ozil, majeruhi ya Podolski ni poigo kwa Wenger ambaye amekwishakamilisha kikosini.
 
Olivier Giroud na Theo Walcott ndio washambuliaji pekee wa kati waliobaki kwenye kikosi cha  Wenger, na mchezaji mpya Yaya Sanogo ndiye anakuwa wa akiba pekee.
 
At the double: Podolski recently scored two goals in a Premier League win against Fulham
Mawili: Podolski hivi karibuni ameifungia Arsenal mabao mawili katika mchezo dhidi ya Fulham Ligi Kuu ya England

No comments

Powered by Blogger.